Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) kabla ya kutoa elimu ya mpiga kura kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akieleza jambo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge na katikati ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Bw. Hassan Bendeyeko.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge vitabu vya Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchgauzi wa Rais,Wabunge na Madiwani baada ya kutoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifuatilia elimu ya mpiga kura.
Baadhi
ya wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye
halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifuatilia elimu ya mpiga
kura.
Hussein Makame, NEC
TUME ya
Taifa ya Uchaguzi imesema haitasita kuifutia kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga
Kura Asasi yoyote itakayotoa maneno ya kuleta uchochezi au kupigia debe sera za
chama fulani cha siasa kwani kufanya hivyo kukiuka matakwa ya Kisheria.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.
Emmanuel Kawishe wakati akijibu swali la mmoja wa wajumbe wa mkutano wa kamati
ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma leo.
Mjumbe huyo
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stela
Manyanya alitaka kufahamu Tume ina utaratibu gani kuhakikisha baadhi ya Asasi
zinazofadhiliwa kutoa elimu ya mpiga kura kutumia nafasi hiyo kuhasisha sera za
chama fulani.
Bw. Kawishe
alisema Kifungu cha 4 (C) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimeipa mamlaka Tume
kuzipa kibali Asasi na kuzisimamia na kuratibu
Elimu ya Mpiga Kura na haitasita
kufuta kibali hicho iwapo masharti yatakiukwa.
“Tume
ikishatoa kibali inafanya ufuatiliaji na tathmini.Tumekwambia nenda katoe elimu
ya mpiga kura..lazima tutafuatilia ili kuona kwamba unachotakiwa kusema
ndicho.Lakini kwa sababu tu umetoa uchochezi Tume ndiyo imekupa kibali na Tume
ndiyo yenye mamlaka ya kukunyima icho kibali” alisema Bw. Kawishe na kuongeza:
“Kwa hiyo
kwa kuwa Tume haina uwezo wa kifedha inaruhusu Asasi zijitegemee lakini
zikishaenda kwenye siasa tutazinyia icho kibali na kibali kitafutwa kwa sababu
Tume ina mamalaka hayo Sheria inaturuhusu Kifungu cha 4 (C) cha Sheria ya Taifa
ya Uchaguzi kimeipa mamlaka Tume kuzipa kibali Asasi na kuzisimamia na kuratibu
Elimu ya Mpiga Kura na haitasita kufuta
kibali hicho iwapo masharti yatakiukwa.”
Kwa uapnde
wake Kamishna wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mary Longway amewataka wajumbe wa
mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma kufikisha elimu ya mpiga kura
kwa wananchi wao ili wafahamu mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi mkuu.
Jaji Mst.
Longway aliyasema hayo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwa wajumbe wa mkutano
huo kwenye uliofanyika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma.
Alisema kwa
sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatekeleza matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni
ya kutoa elimu ya mpiga kura katika kipindi chote cha mwaka leongo ni kuwahamasisha
wananchi kutumia haki yao ya kikatiba na kujitokeza kushiriki kuchagua viongozi
wao.
“Elimu hii
inawajengea wananchi ufahamu na ulelewa kuhusu haki na wajibu wao katika
kushiriki katika na wawezesha wananchi na wadau wa uchaguzi kupata taarifa
sahihi kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani” alisema Jaji
Mst. Longway na kuongeza:
“Tunawaomba
wajumbe wa mkutano huu muende mkafikishe elimu hii ya mpiga kura kwa wananchi
mnaowaongoza ili wafahamu mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi mkuu na
kutekeleza haki na wajibu wao kikamilifu”
Katika
mkutano huo wajumbe kutoka halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma walipata elimu ya
mpiga kura na kuuliza maswali ambayo yalijibiwa.
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi inatoa elimu ya moiga kura kupitia njia mbalimbali ili
kutekeleza matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni zinazoongoza majukumu ya Tume
ambapo mbali na kutoa elimu katika mkutano huo ilitarajiwa kutoa elimu kwenye
Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Sengea.








No comments:
Post a Comment