TANGAZO


Thursday, November 17, 2016

KIKWETE KUWA MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA 46 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete (kulia), akiwa na Makamu wake, Prof. Rwekaza Mukandala

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam   Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 46 ya Chuo hicho Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere Mlimani yatakayofanyika tarehe 19 mwezi huu katika ukumbi wa Mlimani City saa 4 asubuhi Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari na kusainiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala,   inasema wahitimu hao ni wa kundi la pili ambalo linawahusu wahitimu wa Shahada za awali zilizobakia kutoka Ndaki ya Habari na Teknolojia za Mawasiliano (CoICT), Ndaki ya Sayansi za Jamii (CoSS), Ndaki ya Insia (CoHU) na Shule kuu ya Elimu (SoED).

Ndaki nyingine ni Shule Kuu ya Masomo ya Biashara (UDBS),Shule kuu ya Sheria (UDSoL), Shule kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI).

Taarifa hiyo inaongeza kuwa katika mahafali hayo mgeni rasmi atatunuku Shahada,Stashahada na Vyeti kwa Wahitimu.

No comments:

Post a Comment