Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akizungumza katika hafla fupi ya kumkabidhi tuzo na kumvisha nishani Dkt. Fredrick Kigadye aliyotunukiwa na Baba Mtakatifu Papa. Francis mapema wikiendi hii. Kushoto ni Mwadhama Kardina Polycarp Pengo, Dkt Fredrick Kigadye na Mkewe.
Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo akimkabidhi hati yenye ujumbe maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu Papa. Francis Dkt. Fredrick Kigadye wakati wa hafla ya kumkabidhi tuzo aliyetunukiwa kufuatia mchango wake mkubwa katika kulitumikia Kanisa Katoliki kupitia Idara ya Afya chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) mapema wikiendi hii. Kulia ni Mke wa Dkt. Kigadye akishuhudia tukio hilo.
Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo akimvalisha nishani ya heshima ijulikanyao kwa jina la Benemerenti (Anayestahili) Dkt. Fredrick Kigadye aliyetunukiwa tuzo hiyo na Baba Mtakatifu Papa Francisco kufuatia mchango wake mkubwa katika kulitumikia Katisa Katoliki kupitia Idara ya Afya chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mke wa Dkt. Kagadye akishuhudia tukio hilo.
Dkt. Fredrick Kigadye akitoa neon la shukrani kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa kutambua mchango wake katika jamii na kanisa kwa ujumla.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Maaskofu wa
Katoliki Tanzania (TEC) Padre Raymond Saba akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Fredrick Kigadye wakati wa hafla ya
kumkabidi tuzo mapema wikiendi hii Jijini Dar es Salaam.
Na Frank Shija,
MAELEZO
12/11/2016
JAMII imetakiwa kufanya
kazi kwa uadilifu, uaminifu, weledi na uzalendo wa hali ya juu ili wapate
kuheshimika na kuthaminiwa na jamii zinazowazunguka kwa kutambua mchango wao
katika kuendeleza jamii.
Hayo yamesemwa na
Mwadhama Kardinali Polycup Pengo wakati wa hafla ya kumkabidhi nishani ya Benemerenti (Anayestahili), Dkt. Fredrick Kigadye, ambayo
utolewa na Baba Mtakatifu kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kulitumikia Kanisa
na jamii kwa ujumla jana Jijini Dar es Salaam.
“Ni vyema tukatambua
ya kwamba kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio
mahali pepote pa kazi na katika maisha yetu ya kila siku”. Alisema Kardinali
Pengo.
Kwa upande wake Rais
wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa masema
kuwa Dkt. Kigadye amekuwa mtumishi wa wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa
muda wa miaka 35 huku akifanya kazi katika Idara ya Afya katika Hospitali ya Rufaa
ya Bugando kwa mafanikio makubwa.
Ameonesha ni namna
gani watu tunapaswa kujitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu kupitia vipawa na
taaluma tulizo jaaliwakuwa nazo hii inatia moyo sana. Aliongeza Askofu
Ngalekumtwa.
Akizungumzia Tuzo
hiyo aliyopewa na Baba Mtakatifu Papa Francis, Dkt Kagadye amesema kuwa
anajisikia mwenye furaha kubwa na wathamani kwa kupewa tuzo ya heshima na
kiongozi mkubwa duniani nakuongeza kuwa tuzo hiyo inamuongezea chachu ya kuishi
katika misingi imara ya maadili na weledi.
Aidha alitumia fursa
hiyo kutoa raia kwa watanzania wengine hasa walei wa Kanisa Katoliki kutekeleza
majukumu yao kwa kujituma zaidi ili kuwahudumia wana jamii wanaohitaji huduma
za kanisa ikiwemo elimu, afya na nyingi nyingi.
Dkt. Fredrick Kigadye
amekuwa mtanzania wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo baada ya BABA Mtakatifu Fransisko kukubali maombi ya
Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ya kumtunuku tuzo ya heshima aliyekuwa mkuu
wa idara ya afya mstaafu wa Baraza hilo Dkt. Fredrick Kigadye kutokana na
mchango mkubwa alioutoa kwa kanisa katoliki na baraza akiitumikia idara hiyo na
majukuu mengine.
Tuzo hiyo 'BENEMERENTI'
ilipokelewa kwa furaha na Katibu Mkuu wa TEC Padri Raymond Saba ambaye pamoja
na kumpongeza Dkt. Kigadye, amesema watumishi wengine wa baraza lazima waige
mfano wa utendaji wake.
Historia ya tuzo hiyo
ilianzia miaka ya 1775 enzi za Papa Pius wa VI alipto watunuku tuzo ya
Benemerenti wanajeshi waliokuwa wakitetea ukristu enzi hizo na baadaye mwaka
1925 ndipo ikaamuliwa kuwa tuzo hiyo itolewe kwa yeyote atakayekuwa ametoa
mchango mkubwa kwa kanisa Katoliki na jamii kwa ujumla kupitia majukumu yake ya
kazi za kila siku.


No comments:
Post a Comment