Makamu wa Pili wa Rauis wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimjulia hali Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri aliyelazwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili Jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu kutokana na kudhoofika kwa afya yake. Kati kati yao ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akimpa pole Mhe. Balozi Mapuri aliyelazwa Hospitali ya Muhimbili akipatiwa matibabu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole Bibi Shekha Mohammed Salum, kizuka wa Mbunge wa Jimbo la Dimani marehemu Hafidh Ali Tahir hapo matangani Kijijini kwa Mbunge huyo, Maungani, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kulia kwa Balozi Seif ni kaka wa marehemu Hafidh Tahir, Ndugu Shibu Ali Tahir.
Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mama wa Marehemu Hafidh Ali Tahiri Bibi Mwanapili Juma Khamis wakati alipofika
matangani kuipa pole Familia hiyo akitokea Jijini Dar es Salaam Kikazi. Kulia ya Bibi Mwanapili Juma ni Mkurugenzi wa Redio Bahari FM ambae ni mtu aliyefanya kazi kwa miaka mingi pamoja na Marehemu Hafidh Ndugu Yussuf
Omar Chunda. (Picha zote na Hassan Issa – OMR – ZNZ)




No comments:
Post a Comment