Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto), akiangalia jinsi mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa unavyofanyakazi katika kutoa tarifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo.
Wadau mbalimbali wa vyakula na dawa wakifuatilia kwa makini maelezo
ya Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi
wa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa uliyofanyika hivi karibuni Jijini
Dar es Salaam.
Na
Ally Daud-MAELEZO
WANANCHI
wametakiwa kutoa taarifa pale wanapohisi wamepata madhara ya dawa
wanazozitumia ili kuirahisishia Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na
Dawa (TFDA) kuchukua hatua stahiki zidi ya watengenezaji wa dawa hizo, ili
zisiendelee kuwadhuru wananchi.
Hayo, yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwenye hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya
dawa uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri Ummy amesema kuwa wananchi wawe mstari wa mbele katika kutoa taarifa pindi wanapohisi kupatwa
na madhara ya dawa wanazozitumia ili kuirahisishia TFDA kuchukua hatua stahiki kutokana
na taratibu na sheria zilizopo za kuondoa madawa fekin chini.
“Napenda
kusisitiza kwa wananchi wote kutoa taarifa pale wanapohisi wamepata madhara ya
dawa ili kuirahisishia TFDA kuchukua hatua stahiki kutokana na
utaratibu na sheria zilizowekwa,” alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa bila taarifa hizi
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia TFDA
itashindwa kuchukua hatua muafaka na za haraka katika kudhibiti madhara
yanayotokana na matumizi ya dawa na hivyo kuendelea kusababisha athari kwa watumiaji.
Waziri Ummy amesema kuwa wataalam wa afya na wananchi
wote kwa ujumla wanatakiwa kutoa taarifa
za madhara ya dawa kwa wakati,kwa wale wenye simu zilizounganishwa kwenye
“internet” watumie simu hizo kutoa taarifa za madhara ya dawa, na wale wenye
kompyuta zilizounganishwa kwenye “internet” watumie kompyuta hizo na wale wasio
na simu wala kompyuta zilizounganishwa kwenye “internet “waendelee kutoa
taarifa kwa kutumia fomu za njano na kijani.
Mbali na hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa ujazaji wa taarifa hizo kwa kutumia njia za kielektroniki kunasaidia kujua dawa zipi ni sahihi na zipi sisahihi kwa matumizi
ya binadamu na hivyo kuchukua hatua inayostahili.
“Napenda kuwaambia wananchi wajaze fomu hizo ili kutoa taarifa za madhara
ya dawa wanazozitumia ili kufahamu dawa zipi ni sahihi kwamatumizi ya
binadamu na kama sio sahihi basi tuzichukulie hatua zinazostahili,” alisemaBw. Sillo.
Aidha, Bw.
Sillo amesema kuwa moja ya hatua ambayo zitachukuliwa pindi taarifa za madhara ya
dawa zinapotolewa ni kufungia kiwanda kinachotengeneza aina hiyo ya dawa au
kusimamisha matumizi yake ili kuondoa dawa zinazoleta madhara kwa Watanzania.

No comments:
Post a Comment