Pages

Monday, October 24, 2016

Sanches amshinda Rashford tuzo ya mchezaji bora chipukizi Ulaya

Renato Sanches

Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionSanches alichezea Ureno mara sita Euro 2016, na kuwafungia bao moja
Kiungo wa kati wa Bayern Munich Renato Sanches amemshinda mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashfordna kushinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi Ulaya.
Sanches, 19, amewafuata Wayne Rooney, Raheem Sterling, Lionel Messi na Sergio Aguero katika kushinda tuzo hiyo ambayo kwa Kiingereza hufahamika kama Golden Boy na hutunukiwa mchezaji bora Ulaya wa chini ya miaka 21.
Rashford na mchezaji mwenzake Sanches Bayern Munich Kingsley Coman walikuwa wanapigania tuzo hiyo na Sanches.
Nyota huyo atakabidhiwa tuzo hiyo katika hafla itakayofanyika Monte Carlo Jumatatu.
TuttosportImage copyrightTUTTOSPORT
Image captionWanahabari kutoka vyombo 30 vya habari Ulaya hupiga kura. Tuzo hiyo hudhaminiwa na gazeti la Italia la Tuttosport
Tuzo hiyo ilianzishwa na gazeti la Tuttosport mwaka 2003.
Sanches alijiunga na Bayern Munich majira ya joto mwaka huu kwa £27.5m na amewachezea mechi nane msimu huu.
Amechezea Ureno mechi 11.
Alicheza Euro 2016 akiwa na miaka 18 na kuwa mchezaji wa umri mdogo zaidi kuchezea timu iliyoshinda.
Aidha, alishinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment