Mfalme wa Thailand Bhumibol Adulyadej, mfalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88, ikulu ya nchini hiyo imetangaza.
Alikuwa ametawala kwa miaka 70.
Mfalme huyo alienziwa sana nchini Thailand na amekuwa akitazamwa kama nguzo kuu ya kuunganisha taifa hilo ambalo limekumbwa na misukosuko mingi ya kisiasa na mapinduzi ya serikali.
Alikuwa amedhoofika sana kiafya miaka ya karibuni na hajakuwa akionekana hadharani sana.
Kifo chake kimetokea huku Thailand ikisalia chini ya utawala wa kijeshi kufuatia mapinduzi yaliyotekelezwa 2014.
Ikulu ilikuwa awali imeonya kwamba hali yake ya afya ilikuwa imedhoofika zaidi Jumapili.
Raia wa Thailand wamekuwa wakivalia mavazi ya rangi ya waridi kumtakia heri.
Mamia walikusanyika nje ya hospitali ambapo alikuwa akitibiwa.

No comments:
Post a Comment