Wanafunzi wa Shule ya Sekondali ya Kata ya Mwendakulima iliyoko Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakiimba katika Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike liliofanyika jana katika Shule hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akikabidhi watoto wa kike zawadi ya pedi ambazo zinaweza kufuliwa na kutumika tena baada ya kuwa zimeisha tumika. Pedi hizo zinatolewa kwa msaada wa shirika la Msalaba Mwekundu Mkoani Shinyanga kwa ajili ya watoto wakike wanaotoka kwenye kaya masikini.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akipokewa kwa zawadi ya ua mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Mwendakulima kuhadhimisha Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike liliofanyika katika Shule ya hiyo Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondali ya Kata ya Mwendakulima iliyoko Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wakiimba wakati wa Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike liliofanyika jana katika shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainabu Rajab Telack akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo kipya cha AGAPE kituo kinacholea watoto waliokolewa kutoka ndoa na mimba za utotoni.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainabu Rajab Telack pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Sihaba Nkinga wakiwasili katika kituo cha kulelea watoto walioepushwa na ndoa za utotoni cha AGAPE kilichopo mjini Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Rajab Telack akikabidhi pedi zinazofuliwa kwa mwanafunzi uku katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akikabidhi akishuudia tukio hilo wakati wa tamati ya kilele cha mahadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaliyofanyika mjini Shinyanga mapema jana.

No comments:
Post a Comment