Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto), akikabidhiwa fedha taslim na mmoja wa wananchi wakati wa harambe iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dkt. Ayoub Rioba
Waziri Nape Nnauye akizungumza na Maofisa wa Kampuni ya Ving'amuzi ya StarTimes, wakati wa hafla hiyo.
Waziri Nape akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa StarTimes.
Waziri Nape akikabidhiwa mfano wa hundi ya sh. milioni 10 na mmoja wa viongozi wa Kampuni ya StarTimes.
Waziri Nape Nnauye akizungumza na Maofisa wa Kampuni ya Ving'amuzi ya StarTimes, wakati wa hafla hiyo.
Waziri Nape akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa StarTimes.
Waziri Nape akikabidhiwa mfano wa hundi ya sh. milioni 10 na mmoja wa viongozi wa Kampuni ya StarTimes.
Waziri Nape akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Na Anitha Jonas – whusm
22/09/2016
Dar es Salaam.
ZAIDI ya Shilingi Milioni thelathini za kusanywa katika kuwasaidia wa athirika wa Tetemeko la Ardhi Kagera.
Kiasi hicho cha Pesa kilikusanywa jana jijini Dar es Salaam katika Harambee iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa ajili ya ilikuwasaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.
Akizungumza katika ufunguzi wa Harambee hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye aliwataka watanzania kulichukulia suala Maafa ya Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera kuwa nila kila mtanzania na kutoa wito wakujitoa kuchangia chochote kunusuru hali ya watu waliyoathirika pamoja na miundombinu.
“Ninawaomba watanzania wote na wasio watanzania kujitokeza kutoa misaada kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko hili,pia ombi langu kwa wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia kuboresha miundombinu iliyoharibika ikiwemo,Shule,Barabara na Makazi ya wananchi wa Kagera kwa kufanya hivyo kutasaidia kurudisha furaha kwa wakazi hao,”alisema Mhe.Nnauye.
Akiendelea kuzungumza katika Harambee hiyo Mhe.Nnauye alipongeza uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa kuandaa Harambee hiyo kwani kwa kufanya hivyo wameonyesha kuguswa na maafa hayo ya Tetemeko.
Kwa upande wa mmoja wa wadau waliyohudhuria harambee hiyo kutoka Kampuni ya Startimes Bw.Juma Sharobaro alitoa wito kwa watanzania kuungana kwa umoja na kuwasaidia waathirika hao wa tetemeko kwa kutoa mfano wanchi yao ya China kuwa ilishawahi kupatwa na maafa ya tetemeko kama hilo na liliuwa watu wengi lakini walijiunga kwa umoja kutoa msaada kwa waathirika.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Rioba alisema kuwa Harambee hiyo ni endelevu na aliwasihii watanzania kujitokeza na kuchangia kwa kiasi chochote kulingana na uwezo wako kwani haba na haba hujaza kibaba na uhitaji wa msaada mkoani Kagera ni mkubwa.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa Shirika la Utangazaji la Taifa alizitaja namba ambazo mtu yeyeto anaweza kutuma mchango wake kuanzia jana kuwa kwa upande wa benki ni kupitia Akaunti ya namba ya CRDB Benki ambayo ni 15222561730,Tigopesa 0718 069616,Mpesa 0768 196 669 na Airtel Money 0682 950009 na kusema kwa kuchangia kiasi chochote kupitia namba hizo kutawasaidia sana wakazi wa Kagera.
Hata hivyo ilielezwa kuwa msaada wowote unapokelewa na shirika hilo ukiwemo wa vyakula na mahitaji mengine ambayo mtu yoyote atakuswa kuchangia kwa wakazi hao.
No comments:
Post a Comment