Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene akizungumza katika hafla ya kuwaapisha Wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Manispaa na Wilaya 13 walioteuliwa hivi karibuni. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki, Naibu Waziri Selemani Jafo, baadhi ya wakurugenzi, wafanyakazi kutoka OR-TAMISEMI pamoja na waandishi wa habari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Angella Kairuki akiongea Wakurugenzi wapya mara baada ya kuapishwa leo mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene. Kushoto kwa Simbachawene ni Mkurugenzi mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilimanjaro Bi. Butamo Nuru Ndalahwa.
Baadhi ya Wakurugenzi wa halmashauri wakisaini hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa umma pamoja na ahadi ya kuwa waaminifu na wazalendo kwa nchi yao leo katika ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma mbele ya Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Kanda ya Kati Cathlex Makawia.
Baadhi ya Wakurugenzi wa halmashauri wakisaini hati ya kiapo cha maadili ya utumishi wa umma pamoja
na ahadi ya kuwa waaminifu na wazalendo kwa nchi yao leo
katika ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma mbele ya Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Kanda ya Kati Cathlex Makawia.
Na
Nasra Mwangamilo- Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
Mhe. George Simbachawene amewaasa
Wakurugenzi wapya kusimamia mapato ya ndani katika halmashauri zao ili waweze
kutekeleza miradi ya maendeleo na kuwahudumia wananchi.
Waziri
Simbachawene amesema
hayo leo mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Wakurugenzi wapya 13
walioteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli iliyofanyika katika jengo la Mkapa, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mkoa na Serikali za Mitaa mjini Dodoma. Pamoja na kuapishwa, Wakurugenzi hao
walikula kiapo cha maadili ya utumishi wa umma pamoja na ahadi ya kuwa
waaminifu na wazalendo kwa nchi yao.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Waziri
Simbachawene alisema Wakurugenzi
hao wanawajibu wa kusimamia mikataba iliyopo, iliyopita na itakayoingiwa na
halmashauri zao ikiwa ni pamoja na kuzingatia
masharti ya mikataba hiyo wakati wa utekelezaji wake. Aidha, aliwahimiza kuwa
wawajibikaji kwa mamlaka waliyonayo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu
zilizowekwa kikatiba.
“Kuanzia
leo mnaitwa viongozi, unapokuwa kiongozi unalazimika kuishi kwa namna tofauti
kabla ya kuapishwa kuwa kiongozi, eneo mnaloenda kufanya kazi ni muhimu na
mnaenda kuongoza taasisi na mnaenda kuwahudumia wananchi moja kwa moja” alisema
Simbachawene.
Waziri
Simbachawene amewaeleza
Wakurugenzi hao kuwa unapozungumzia kuondoa umasikini wa wananchi, Mkurugenzi
ndiye anayebeba bendera na dhamana ya kusimamia sekta zote ndani ya halmashauri
ikiwemo afya, kilimo, elimu, maji, uvuvi ambazo zitawaletea hali bora ya maisha
ya wanachi hao.
Katika
kuyatekeleza majukumu hayo, Waziri Simbachawene
amewahimiza wakurugenzi hao kufanya kazi na Wizara zote kwa kufutata sera
mbalimbali na miongozo inayotolewa na viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
Aidha,
Waziri
Simbachawene amewataka
Wakurugenzi hao kutembelea maeneo yao katika halmashauri zao badala ya kukaa
ofisini kuanzia tarehe 1 hadi 30 kila mwezi ili kujionea changamoto
zinazowakabili wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
“Tokeni
ofisini na tembeleeni maeneo yenu, mna mambo mengi ya kufanya, ni lazima uwajue
wananchi, viongozi unaofanya nao kazi, taasisi na watumishi wako kwa takwimu
ikiwezekana kwa majina” alisisitiza Waziri Simbachawene.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Angellah
Kairuki amewataka Wakurugenzi hao wafuatilie na kusimamia miradi ya maendeleo
iliyopo ndani ya halmashauri zao kwa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha
zilizotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Kuhusu
watumishi hewa, Waziri Kairuki amesema kuwa hadi sasa wamebainika watumishi hewa
17,102 tangu kuanzishwa zoezi hilo Machi mosi mwaka huu na kuwaasa wakurugenzi
hao kufuatilia watumishi ndani ya halmashauri zao ili kuondokana na dhana ya
kuwa na watumishi hewa ndani ya halmashauri zao.
Ili
kuwa na taarifa sahihi, Waziri Kairuki amewataka Wakurugenzi hao watumie mifumo
sahihi ili kutoa taarifa sahihi za watumishi na kuondoa dhana ya watumishi hewa
ndani ya halmashauri zao.
Kwa
upande wao Mkurugenzi mpya wa halmashauri
ya wilaya ya Bukoba Mwantumu Dau na Frank Bahati wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ukerewe wamemshukuru Rais kwa kuwateua na kuhahidi kutomuangusha ambapo na
watawatumikia wananchi kwa nguvu zao zote katika kuwaletea maendeleo.
Wakurugenzi
13 wa Halmashauri za Manispaa, Mji na Wilaya walioapishwa na Katibu Msaidizi
Sekretarieti ya Maadili ya Vingozi wa Umma, Ofisi ya Kanda ya Kati Cathlex
Makawia ni pamoja na Godwin Emmanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma, Elias R.
Ntiruhungwa Mji waTarime, Mwantumu Dau Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Frank
Bahati Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya
Wilaya ya Mbulu, Mwailwa Smith Pangani Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Godfrey
Sanga Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na Yusuf Daudi Semuguruka Halmashauri
ya Wilaya ya Ulanga.
Wakurugenzi
wengine ni Bakari Kasinyo Mohamed Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Juma
Ally Mnweke Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Butamo Nuru Ndalahwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Waziri Mourice
Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na Fatma
Omar Latu Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.






No comments:
Post a Comment