Viongozi wa nchi wanachama wa muungano wa maendeleo Afrika Mashariki na pembe ya Afrika (IGAD) wanatarajiwa kukutana katika mkutano wa kihistoria mjini Mogadishu, Somalia.
Itakuwa mara ya kwanza kwa mkutano kama huo kufanyika mjini Mogadishu tangu kuanzishwa kwa muungano huo miaka 30 iliyopita.
Wengi wa wanachama, Ethiopia, Uganda na Kenya, wamechangia wanajeshi katika kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika ambacho kinasaidia serikali kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabab.
Mikutano kama hiyo haingeweza kufanyika katika mji huo kwa karibu mwongo mmoja uliopita kwa sababu za kiusalama.
Mwandishi wa BBC aliyeko Mogadishu Ibrahim Aden anasema ulinzi mkali unadumishwa katika mji huo na barabara nyingi kuu zimefungwa.

No comments:
Post a Comment