Pages

Tuesday, September 13, 2016

TAARIFA YA TBC: SAFARI YA DODOMA JUMATANO HII, BALOZI LIUNDI KUNGURUMA

Balozi Christopher Liundi

Habari,
TBC imekuwa ikirusha kipindi cha "Safari ya Dodoma" kila Jumatano saa 3 usiku na marudio yake yakiwa Alhamisi saa 2 asubuhi na Ijumaa saa 3:30 usiku. Katika kipindi cha wiki hii, yaani Jumatano ya tarehe 14 September 2016, tutakuwa na majadiliano ya Uchumi wa mkoa wa Dodoma kutoka kwa wawekezaji wa viwanda vidogo vidogo, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alipotembelea makazi yake mapya ya mjini Dodoma, pia katika studio zetu za TBC tutakuwa na mgeni wetu, Balozi Christopher Liundi, mwanadiplomasia wa muda mrefu na aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Usikose kuangalia kipindi hiki. Jumatano tarehe 14 Sept. Saa 3 usiku TBC1

Godfrey Semwaiko
Mratibu wa Kipindi.

No comments:

Post a Comment