Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu yao hiyo dhidi ya Mtibwa Sugar, uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo jioni. Katika mchezo huo Simba imeshinda mabao 2-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwinyi Kazimoto (kushoto) wa Simba akiwania mpira uliokuwa ukidhibitiwa na Salim Abdallah wa Mtibwa Sugar wakati wa mchezo huo.
Janvier Bukungu wa Simba akipiga mpira krosi huku akifuatwa na Kelvin Idd wa Mtibwa Sugar.
Ibrahim Ajib wa Simba akiudhibiti mpira hukua akibanwa na Said Mkopi wa Mtibwa.
Jamal Mnyate (kulia) wa Simba akiwania mpira na Kassian Ponera (kushoto) wa Mtibwa Sugar.
Hapa ilikuwa ni heka heka langoni kwa Mtibwa Sugar.
Ibrahim Ajib wa Simba akifunga bao la kichwa likiwa ni bao la kwanza kwa timu yake hiyo katika mchezo huo.
Ibrahim Ajib akishangilia bao hilo.
Ibrahim Ajib (katikati), akishangilia bao hilo na Laudi Mavugo (kushoto) na Mohamed Hussein 'Shabalala'.
Laudit Mavugo akishangilia baada ya kuifungia timu yake ya Simba bao la pili katika mchezo huo.
Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib wakishangilia bao hilo.
Blagnon wa Simba kiwania kuupiga mpira kichwa huku ukinaswa na beki Salim Abdallah wa Mtibwa Sugar.
Jamal Mnyate wa Simba akiudhibiti mpira kwa kichwa huku akifuatwa na Kassian Ponera wa Mtibwa Sugar huku mpira ukiwa umefikia mwisho na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
No comments:
Post a Comment