Waziri
wa Habari, Utaamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akiwaeleza jambo
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa (Katikati)na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene wakati wa kikao cha bunge leo
Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha bunge leo Mjini Dodoma. Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu swali wakati wa kikao cha bunge na kuahidi kuwa serikali kuendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali nchini ikiwemo upatikanaji wa madawa na vifaa tiba.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiwaeleza wabunge mipango ya Serikali kuendelea kushughulikia changamoto za nishati ya umeme nchini hasa katika maeneo ya Lindi na Mtwara.
Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge mapema leo.
Naibu
Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali kwa wabunge
ambapo alisema kuwa Serikali inafanya kila jitihada ya kuwaongezea uwezo katika
watendaji wake ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia nchini.(Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)







No comments:
Post a Comment