TANGAZO


Thursday, September 8, 2016

DC WA HANDENI GODWIN GONDWE ASULUHUSHA MGOGORO WA MPAKA ULIODUMU KWA MUDA MREFU

Mkuu wa Wilaya ya Handeni (wa kwanza kushoto), Godwin Gondwe, akisoma ramani ya mwaka 2007 akiwa na viongozi na wananchi ili kujua mpaka upo sehemu gani. DC Gondwe amefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa mpaka uliodumu kwa muda mrefu akiwa ameambatana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili uliohusisha Kijiji cha Kweditilibe cha Handeni Vijijini na kitongoji cha Makinda kilichopo Handeni Mjini.

RAMANI YA 2007  ndiyo iliyotumika kusuluhisha mgogoro huo ambapo aliwaeleza wananchi kuwa ramani hiyo ndiyo iliyotumika kuweka mipaka ya maeneo husika Tanzania nzima na hakuna mwenye mamalaka ya kuibadili isipokua Rais mwenye mamalaka ya Ardhi ya Tanzania nzima.
Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe akisalimiana na mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Handeni kabla ya zoezi la kutatua mgogoro wa mpaka.

No comments:

Post a Comment