Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bibi. Joyce Fissoo
Na Frank Shija, Maelezo
13/09/2016
SERIKALI
imepongeza juhudi za wadau wa Tasnia ya Filamu nchini kutokana na jitihada zao
katika kuhakikisha tasnia hiyo inakuwa na kuwaletea maendeleo endelevu ikiwemo
Ajira za uhakika kwa vijana.
Pongezi
hizo zimetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) Bibi.
Joyce Fissoo alipokutana na ujumbe kutoka Taasisi isiyo ya Kiserikali ya TYEOO
walipomtembelea ofisini kwake jana kwa ajili ya kutambulisha rasmiMradi wa
TYEEO Barazani entertainment jana Jini Dar es Salaam.
Fissoo
alisema kuwa mradi huo ni muhimu kwa mustakabari wa kukuza tasni ya Filamu
nchini kwani utarahisha kufikisha katika kuwafikia wadau wengi zaidi wa tasni
hiyo walioko katika mikoa ya pembezoni.
“Niseme
tu kwa dhati kabisa nawapongeza sana kwa ubunifu wenu mradi huu ni mzuri na
utaongeza tija katika tsni yetu ya Filamu, name nina waahidi kuwapa ushirikiano
pindi mtakapo kuwa mnahitaji”. Alisema Fissoo.
Aidha
alitoa ushauri kwa Taasisi hiyo kutumia vibanda vya maonyesho ya Filamu
vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini ili kutekeleza mradi huo kwa kuwa nia
ya Serikali ni kuona dhana ya urathimishaji wa kazi za wasinii inafanikiwa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TYEEO, John Kallaghe amesema kuwa pamoja na
kuwa mradi huo ni binafsi lakini kutokana na imani kubwa waliyonayo juu ya Bodi
ya Filamu wameona siyo busara kuendelea kutekeleza jambo kubwa kama hili bila
ya kushirikisha mamlaka hiyo ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa Tasnia ya Filamu
nchini.
Aliongeza
kuwa wazo la kuanzishwa kwa mradi huu ilikuwa ni kusaidia kuwawezesha vijana
kujikomboa katika lindi la umaskini kupitia huduma itokanayo na mradi huu
ambayo ni utayarishaji na usambazaji wa kazi za wasanii wa Filamu kwa njia ya
kisasa zaidi.
Kallaghe
alisema kuwa wao kama wadau tasni hiyo wako tayari kupokea ushauri na maelekezo
ya namna ambavyo wanaweza kuboresha na kutekeleza mradi huo kwa ajili ya
maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Mradi
wa TYEEO Barazani ni miongoni mwa miradi kadhaa ambayo imeanzishwa na taasisi
ya TYEEO, ulioasisiwa tangu mwaka 2013 na unakadiriwa kutoa fursa ya ajira za
uhakika kwa vijana takribani 6000 katika
kada zote za Filamu hadi kufikia mwaka 2017.


No comments:
Post a Comment