TANGAZO


Thursday, August 18, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU AMUAGA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA IDADI YA WATU DUNIANI (UNFPA) LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni Dk.Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto)  akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) mara baada ya kufika Ofisini kwake kumuaga leo jijini Dar es salaam.Wengine alioambatana nao ni Mratibu Mkazi  wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto).
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) kuhusu machapisho mbalimbali ya Umoja  yanayoelezea Maendeleo ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa Shirika hilo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.)akiangalia moja ya chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021 alilokabidhiwa na Mratibu Mkazi  wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (katikati) , Mwakilishi Mkazi wa UNFPA anayemaliza muda wake hapa nchini Dk. Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto), Mratibu Mkazi  wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja  huku wakionesha chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021 leo jijini Dar es salaam. (Picha/Aron Msigwa –Maelezo)

Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) amemuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa Shirika hilo. 

Akizungumza na mwakilishi huyo Ofisini kwake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy ameeleza kuwa Serikali itaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Sera, miongozo na sheria mbalimbali zinazohusu usawa wa jinsia na haki za watoto hususan watoto wa Kike.

Amesema Serikali itaendelea kufanya kazi na kushirikiana na UNFPA pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Tanzania.


Ameleza kuwa wizara yake itaendelea kuhakikisha kuwa tatizo la ukatili dhidi ya watoto linalohusisha ndoa na mimba za utotoni, ubakaji na ulawiti kwa watoto linamalizika katika jamii ya watanzania


Aidha,amesema kuwa wizara yake itaendelea na juhudi za kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa kuweka miundombinu na mazingira bora ya kujifungulia   huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuelimisha na kuhamasisha umma wa watanzania juu ya umuhimu wa kuzingatia uzazi wa mpango.

Kwa upande wake Dk. Natalia Kanem ambaye alikua  ameambatana na Mratibu Mkazi  wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliyompatia katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini na kuahidi kuendeleza kudumisha mashirikiano hayo atakapokuwa Makao Makuu ya Shirika hilo.


No comments:

Post a Comment