Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano, Prof. Faustine Kamuzora akiongea na wataalam wa Tehama wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wanahabari (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa.
Na Abushehe
Nondo, Maelezo.
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ameiagiza Tume ya Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano nchini
kuhakikisha wanatengeneza misingi ya uadilifu wa kitaaluma na misingi hiyo
itumike kuwadhibiti wale ambao wanatumia utaalamu huo kwa nia ovu.
Mhandisi Ngonyani
aliyasema hayo, wakati akizindua mkutano
wa kwanza ambao umeandaliwa ma Tume mpya ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano
(TEHAMA), uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alisema Mkutano huo una
lengo la kuwakutanisha wataalamu wa TEHAMA kutoka katika sekta za umma na sekta
binafsi ili kuweza kujadiliana ni kwa namna gani taaluma hiyo inavyoweza
kutumika zaidi kwa faida ya ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
“Wapo baadhi ya watu
wanatumia taaluma ya TEHAMA kwa manufaa mbalimbali ya kujenga uchumi na
maendeleo, lakini wapo wachache ambao wanatumia utaalamu wao kwa manufaa binafsi ikiwemo kuwadhalilisha watu wengine
na kuwaibia fedha zao katika mitandao” Alisema Mhandisi Ngonyani.
Alisema Tume hiyo ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
inatakiwa kuja na sheria kali ambazo
zitawabana wale wote ambao wamekua na tabia ya kutumia mitandao katika kufanya
vitendo viovu badala ya kutumia katika kujiletea maendeleo.
Awali akizungumza
katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Prof.
Faustin Kamuzora alisema uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini ni jitihada za makusudi za
serikali katika kukuza Mawasiliano.
Prof. Kamuzora alisema
kuwa tume hiyo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa na hivyo
kuwasihi watendaji hao kuwaelimisha zaidi wananchi kujikita zaidi katika kufuata maadili ya
taaluma hiyo ili kulifikisha Taifa katika mafanikio ya sekta ya mawasiliano.
Alisema Tume ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano itasaidia kukuza uchumi wa Taifa kutokana
na kukua kwa sekta ya TEHAMA na kuchochea uzalishaji ,ukuaji wa sekta zingine
kiuchumi na usambazaji wa huduma za jamii.
No comments:
Post a Comment