Meneja
wa Buni Hub Jumanne Mtambalike akifafanua jambo katika Majadiliano yaliyoratibiwa
na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) kwa lengo la kujadili Ripoti
ya Hali ya Ajira kwa Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kazi Dunia
(ILO) jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni muongoza mada Amon Tamilwai. Jukwa
hilo limekuwa likikutana kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo ukutanisha
vijana kwa lengo la kujadili mada mbalimbali zenye muelekeo wa kumkomboa kijana
kifikra.(Picha zote na Frank Shija, Maelezo))
Mratibu
wa Program kutoka Actuality Media Bi. Audrey Fancher akielezea jambo katika
Majadiliano yaliyoratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) kwa
lengo la kujadili Ripoti ya Hali ya Ajira kwa Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa
na Shirika la Kazi Dunia (ILO) jana Jijini Dar es Salaam. Jukwa hilo limekuwa
likikutana kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo ukutanisha vijana kwa lengo la
kujadili mada mbalimbali zenye muelekeo wa kumkomboa kijana kifikra. JUU NA CHINI: Baadhi ya Vijana wakichangia mada katika Majadiliano yaliyoratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) kwa lengo la kujadili Ripoti ya Hali ya Ajira kwa Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) jana Jijini Dar es Salaam. Jukwa hilo limekuwa likikutana kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo ukutanisha vijana kwa lengo la kujadili mada mbalimbali zenye muelekeo wa kumkomboa kijana kifikra.
Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) wakifuatilia mada katika Majadiliano kuhusu Ripoti ya Hali ya Ajira kwa Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) jana Jijini Dar es Salaam. Jukwa hilo limekuwa likikutana kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo ukutanisha vijana kwa lengo la kujadili mada mbalimbali zenye muelekeo wa kumkomboa kijana kifikra.
Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) wakifuatilia mada katika Majadiliano kuhusu Ripoti ya Hali ya Ajira kwa Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) jana Jijini Dar es Salaam. Jukwa hilo limekuwa likikutana kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo ukutanisha vijana kwa lengo la kujadili mada mbalimbali zenye muelekeo wa kumkomboa kijana kifikra.
Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) wakibadilishana mawazo mara baada ya kumaliza Majadiliano kuhusu Ripoti ya Hali ya Ajira kwa Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) jana Jijini Dar es Salaam. Majadiliano hayo yameratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF).
Baadhi ya waratibu wa Jukwaa la
Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF). Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa wa TASEF Adian Nzamba, Mratibu
wa TASEF Bi. Genoveva Emanuel Mtiti na
Mshereheshaji Amon Tamilwai.
Na Frank Shija, MAELEZO.
VIJANA nchini wanatakiwa kujijengea mazoea ya kupenda kujifunza kila wakati ili
kuendelea kuibua mawazo endelevu kwa mustakabari wa maendeleo yao.
Hayo
yamesemwa na Rais wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) Adrian
Nzamba wakati wa majadiliano ya Ripoti ya Hali ya Ajira iliyoandaliwa naShirika
la Kazi la Dunia (ILO) wakati wa majadiliano yaliyoandaliwa na Jukwaa hilo
jana Jijini Dar es Salaam.
“Vijana
tunatakiwa tuwe na moyo wa kujifunza, wengi wetu wamekuwa wazito kujifunza.” Alisema Adrian.
Aliongeza
kuwa kupitia Jukwaa hilo wamekuwa wakiwajengea uwezo Vijana katika hatua ya
kujitambua na kuepukana na mawazo mgando yenye fikra hasi.
Kwa
upande wake Meneja wa Buni Hub mshiriki mwenza wa Jukwaa hilo Jumanne
Mtambalike ameipongeza Serikali kwa mchango wake katika kusaidia Vijana kufikia
malengo yao.
Mtambalike
amesema kuwa wao kama Buni Hub wamekuwa chini ya Tume ya Sayansi Tanzania
(COSTECH) ambayo ni Taasisi ya Serikali hivyo ni dhahiri kuwa Vijana
wakijitambua wanazo fursa nyingi kupitia Serikali yao kwani wao kama taasisi
binafsi lakini wananufaika.
Aliongeza
kuwa lengo kubwa la kushiriki Jukwa hilo ni kuwajengeauwezo vijana wa kufikiri
na kujitegemea badala kukaa na kulalamika bila sababu ya msingi.
“Vijana
tumekuwa na tabia ya kulalamika sana, zipo fursa nyingi tu ili mradi unapata
taarifa tafuteni taarifa zipo fursa nyingi sana binafsi nilipata udhamini wa
kusoma nje ya nchi kupitia Wizara ya Habari kwa sababu nilitafuta taarifa”.
Alisema Mtambalike.
Aidha
alitoa rai kwa Taasisi za Elimu ya Juu kushirikiana na wadau mbalimbali ili
kuangaliana namna ya kuwa na njia bora ya kuwaandaa vijana ili kukidhi mahitaji
ya soko la ajira.
Katika
Jukwaa hilo vijana waliibua hoja mbalimbali zikiwemo kubadilisha mfumo wa Elimu ili kuingiza mitaala ya
Ujasiriamali, vijanga kujishughulisha na utafutaji wa taarifa na msisitizo wa
vijana kushiriki katika kazi za kujitolea.
No comments:
Post a Comment