TANGAZO


Monday, August 15, 2016

TANAPA, NGORONGORO NA IDARA YA WANYAMAPORI SASA KWENDA KIJESHI

Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi za Taifa likiingia katika viwanja vya mazoezi katika kambi ya mafunzo ya Mlele wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (hawapo pichani) wakati wa ufungaji  mafunzo kwa askari na maafisa hao yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi 
Askari na Maafisa wa Hifadhi wakipita kwa heshima mbele ya mgeni rasmi  kwa mwendo wa pole na haraka wakati wa ufungaji  wa mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu kutoka mfumo wa kiraia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakipokea salamu za heshima kwa kupiga saluti wakati gwaride likipita mbele kwa heshima wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari wa shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa Ngorongoro.
Bendi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi, Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Askari na Maafisa wa Hifadhi za Taifa wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Witness Shoo (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko wakifuatilia maonesho ya matumizi ya silaha kutoka kwa wahitimu hao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete akisherehesha wakati wa ufungaji wa mafunzo  ya kijeshi kwa askari na Maafisa wa Hifadhi  waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Askari na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya jeshi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Freddy Manongi wakifuatilia maonesho hayo.

Askari na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitizama matundu ya risasi zilizolengwa na mmoja wa askari wa uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi. 
Wakufunzi wa Mafunzo ya kijeshi kwa maofisa na askari wa Hifadhi za Taifa wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi,(hayupo pichani).
Mhifadhi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Lilian Magoma akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake wa mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa askari na maafisa wa uhifadhi waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Getrude Lyatuu akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro, Freddy Manongi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Alexander Songorwa akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuzungumza na wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maofisa wa Hifadhi za Taifa .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari na maofisa wa Hifadhi za Taifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa katika pichaya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi. (Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog, Kanda ya Kaskazini)

No comments:

Post a Comment