Pages

Saturday, August 20, 2016

Taliban wateka wilaya muhimu nchini Afghanistan

Wapiganaji wa Taliban waliinga mji wa Kunduz mwezi Septemba

Image copyrightREUTERS
Image captionWapiganaji wa Taliban waliingia mji wa Kunduz mwezi Septemba
Wanamgambo wa Taliban wameteka wilaya muhimu katika mkoa ulio kaskazini mwa Afghanistan wa Kunduz.
Wapiganaji hao walishambulia kutoka sehemu tofauti hatua iliyowalazimu wanajeshi wa serikali kurudi nyuma kwenda mji wa Kunduz.
Ukosefu wa risasi na vikosi zaidi vilichangia kutekwa kwa wilaya ya Khanabad.
Wanajeshi wa serikali wanasema kuwa waliishiwa na risasiImage copyrightREUTERS
Image captionWanajeshi wa serikali wanasema kuwa waliishiwa na risasi
Taliban wamepiga hatua tangu vikosi vya kimataifa visitishe shughuli zao mwaka nchini Afghanistan 2014.
Wanajeshi wa Afghanistan kwa sasa wanapigana na wanamgambo hao walio karibu nusu ya wilaya zote 34 nchini humo
Mapema wiki hii Taliban walitaka wilaya moja iliyo mkoa jirani wa Baghlan.

No comments:

Post a Comment