Serikali kupitia
Idara ya Habari-MAELEZO itaanza kutekeleza mikakati mbalimbali inayolenga
kuwapatia wananchi taarifa za kila mara kuhusu utekelezaji wa ahadi zake. Mikakati hiyo itakayosaidia kuongeza uwazi na
ushirikishaji, pamoja na mambo mengine, itahusisha hatua zifuatazo:-
Mosi, kuboresha
mfumo wa mawaziri na watendaji waandamizi Serikalini kuzungumza na wananchi ili
kuainisha utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti, sera na mipango ya Taifa. Kuanzia
Agosti 25 mwaka huu, mawaziri wataanza kuzungumza na umma kupitia vyombo vya
habari kueleza vipaumbele vya bajeti zao na utekelezaji wake hadi kufikia sasa.
Pili, kuanzisha
utaratibu wa Idara ya Habari-MAELEZO kueleza kwa umma kila mara, na haraka
iwezekanavyo, utekelezaji wa sekta zote katika ngazi ya kitaifa. Msemaji Mkuu
wa Serikali atakuwa akitoa taarifa hizo kuanzia hivi karibuni.
Tatu,
Serikali itaimarisha ushirikiano zaidi na wadau mbalimbali katika kutekeleza
mikakati yake ya mawasiliano kwa umma. Pamoja na wadau wengine, Serikali
itahakikisha inafanyakazi kwa karibu na vyombo vya habari ili vishiriki vyema
katika ujenzi wa Taifa.
Mwisho,
wakati huu Idara ikiendelea kufanyiakazi mikakati mingine ili kuboresha
mawasiliano kwa umma, naomba wadau wote kutoa ushirikiano kwangu binafsi, Idara
niliyopewa kuiongoza hivi karibuni na zaidi tumuunge mkono Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Magufuli katika ajenda yake ya mageuzi kupitia HapaKaziTu.
Imetolewa na:
Hassan Abbasi,
Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO.

No comments:
Post a Comment