Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Makonda (kushoto) akifungua kikao chake cha
kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es
salaam.Wengine kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe.
Isaya Mwita na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabida.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Makonda (kushoto) akifungua
kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC)
jijini Dar es salaam.Wengine kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
salaam Mhe. Isaya Mwita na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani
Madabida.
Na Aron Msigwa -
Dar es Salaam.
MKUU wa Mkoa wa Dar
es Salaam Mhe. Paul Makonda amewataka watendaji wa mkoa huo kuhakikisha kuwa wanasimamia
ubora wa madawati yanayotengenezwa na vyumba vya madarasa vinavyojengwa maeneo mbalimbali
ya mkoa huo.
Aidha, amezitaka
manispaa za mkoa huo kuendelea kutenga fedha
kwa ajili ya kujenga madarasa mapya na kuwahamasisha wananchi na wadau
mbalimbali wa maendeleo kujitolea kufanikisha mpango huo na kutoa wito kwa madiwani
kujiwekea mkakati wa kujenga walau madarasa mawili kwenye Kata zao.
Akifungua kikao
chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC), Mhe
Makonda amesema kuwa licha jiji hilo kukabiliwa na changamoto za kimaendeleo za
muda mrefu kwenye sekta ya elimu, miundombinu ya Afya, maji na barabara
mafanikio yameanza kuonekana kutokana na juhudi za pamoja za viongozi wa mkoa
huo.
UPATIKANAJI WA
MADAWATI
Kuhusu upatikanaji
wa madawati amesema kuwa toka Mhe. Rais wa Jamhuri ya Tanzania atangaze kampeni
ya upatikanaji wa madawati kwa ajili ya shule za Msingi kumekuwa na mwitikio
mzuri kwa kutoka kwa viongozi wa mkoa huo wa kuhakikisha madawati yanapatikana.
Amesema mkoa
wake ulikua na upungufu wa madawati zadi ya 66,031 yaliyokuwa yakihitajika
katika shule za msingi huku Sekondari zikihitaji
madawati zaidi ya 30,000.
Amesema wabunge wa
majimbo ya Dar es salaam tayari wametoa madawati 5000 kila mmoja katika yao na juhudi zinaendelea kufanywa na madiwani na Mameya kutenga fedha kwenye bajeti za Halmashauri zao kwa ajili ya ununuzi wa madawati.
Amewashukuru Wakuu wa wilaya kwa kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wananchi na
wadau mbalimbali kuchangia madawati kwa kujitolea na kufanikisha mkoa huo kuwa
umepata madawati yote yaliyobaki ifikapo Agosti 31 mwaka huu.
VYUMBA VYA
MADARASA
Amesema bado
mkoa unakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na kuongeza kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Pombe Magufuli katika ahadi zake aliupatia
mkoa huo kiasi cha shilingi bilioni 2.7 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya
madawati zihamishiwe kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa na kazi ya kumalizia
upatikanaji wa madawati yaliyobaki ibaki kwa viongozi wa mkoa huo.
Amesema fedha
hizo zimekwishakutengwa na kuanza kusambazwa kwenye wilaya husika na kusisitiza
kuwa ujenzi wa madarasa hayo unaendelea lengo likiwa kujenga madarasa 123 kwa fedha
zilizotolewa na Mhe.Rais Dkt. John Magufuli.
“Kama mkoa
tunamshukuru Rais alitupatia shilingi bilioni 2 na akawabana mawaziri wake
wakachanga milioni 107, tukafikisha jumla ya shilingi bilioni 2.1 fedha hizi
ilikua ziende kwenye madawati, nikamwomba Mhe. Rais aturuhusu tuzitumie kwa
ajili ya ujenzi wa madarasa ili madawati tuendelee kupambana nayo sisi wenyewe”Amesisitiza
Mhe. Makonda.
Aidha, wadau
mbalimbali kutoka ndani ya nchi wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kampeni
juhudi za Serikali kwa kutoa michango mbalimbali na kufanikisha ujenzi wa
madarasa kupitia uchangiaji wa mabati mabati 10,000 kwa ajili ya ujenzi wa
madarasa pia wadau kuchangia tani zipatazo 35 za nondo.
USAFI WA
MAZINGIRA.
Amesema mkoa wa
Dar es salaam una changamoto ya uzalishaji wa taka nyingi ikilinganishwa na
maeneo mengine nchini kwa kuwa una idadi kubwa ya watu takribani wakazi zaidi
ya milioni 5 ambao
Amesema juhudi
za kuendelea kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi zinaendelea kwa kuwahamasisha
wananchi kujenga utamaduni wa kusafisha mazingira yao ili kujikinga na magonjwa
ya milipuko ikiwemo kipindupindu
yanayosababishwa na uchafu.
Amewataka
viongozi wa mkoa huo kusimamia wajibu wa kuliweka jiji katika hali ya usafi kwa
kusimamia sheria ili jiji hilo liwe katika hali ya usafi ikiwa ni pamoja na
kuwaagiza wamiliki wa maduka yote katika jiji hilo kuwa na vifaa vya kutupia
taka nje ya maduka yao.
Amepongeza
juhudi za watendaji wa mkoa huo kutenga fedha kwenye bajeti ya 2016/2017 kwa
ajili ya kununulia magari ya kubebea taka.
Ili kuhakikisha
kuwa kampeni hiyo inakuwa endelevu na inafanywa kwa kasi na nguvu kubwa ameanzisha
mpango wa utoaji wa gari (pick-up) na fedha kama motisha kwa Mwenyekiti wa mtaa
atakayefanya vizuri kwenye usafi kuanzia mwezi huu, huku wajumbe 5 wa Serikali
ya mtaa na mtendaji wa mtaa utakaofanya vizuri wakipatiwa kiasi cha shilingi
milioni 5 kila mmoja.
"Napenda
kuwajulisha kuwa mwezi huu niliahidi kukabidhi gari aina ya pick- up kwa mwenyekiti
wa Serikali ya mtaa atakayefanya vizuri kwenye usafi,kwenye mtaaa wake na
tayari nimeshainunua nalenga kutoa motisha kwa viongozi hao” Amesema.
Amesema zawadi
hizo zitatolewa kwa kwa kuzingatia vigezo vya Afya vilivyowekwa na tayari timu
iliyoundwa kufuatilia suala hilo imeanza kazi ya kupita katika maeneo mbalibali
kufuatilia utekelezaji wa kampeni hiyo kubaini mitaa na viongozi waliofanya
vizuri na kusisitiza kwamba viongozi wa mitaa watakaozembea kusimamia usafi
katika maeneo yao watatangazwa hadharani kupitia vyombo vya habari ili jamii
iwajue kuwa wanakwamisha kampeni ya usafi.
SOKO LA KARIAKOO
Mhe. Makonda
amepongeza juhudi zinazofanywa na viongozi na watendaji wa halmashauri ya Ilala
na jiji kuifanya Kariakoo kuwa katika hali ya usafi na na kuwawezesha wananchi
kupita kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali.
Amesema yeye
kama mkuu wa mkoa aliyekabidhiwa jukumu la kusimamia mkoa huo atahakikisha kuwa
maeneo yote ya jiji la Dar es salaam ikiwemo Kariakoo na Ubungo yanabaki kuwa
maeneo yanayowezesha wananchi kupita kwa huru bila hofu yoyote.
“ Mimi
nawapongeza Mameya wa jiji, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na Maafisa Biashara
kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya kuifanya Kariakoo na Ubungo iweze
kupitika, nawahakikishia maadam mimi ndiyo Mkuu wa Mkoa itabaki hivyo, maeneo
hayo yatabaki salama kwa watu kupita na wale wanaofanya biashara na kulipa kodi
wafanye kazi yao kwa uhuru ” Amesisitiza.
WAMACHINGA KATIKATI YA JIJI.
Amewataka wafuate
sheria zinazosimamia jiji kwa kuacha kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa na kuwa
tayari kwenda kwenye maeneo waliyopangiwa na kuongeza kuwa ataendelea kusimamia
sheria, kanuni na taratibu zinazouongoza mkoa huo kuhakikisha kuwa maeneo
yaliyopangwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao na halmashauri husika yanatumika
kama ilivyokusudiwa ili Dar es salaam iwe mahali pazuri na salama pa kuishi.
Mhe. Makonda
amekiri kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wenye maduka eneo la
kariakoo ambao wamekua wakikwamishwa na wafanyabiashara wadogo ambao wamekuwa
wakipanga barabarani, nje ya maduka yao bidhaa zilezile wanazouza wao katika maduka
yao huku wakiwa hawalipii kodi jambo ambalo linawasababishia hasara.
Amewaagiza wakuu
wa wilaya watangaze barabara zitakazotengwa katika kata kwa ajili ya kufungwa mwisho
wa Juma (week end) ili zitumiwe na wafanyabiashara wadogo kama alivyoagiza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa akiwahutubia wakazi wa jiji la
Mwanza Agosti 11, 2016 na kuongeza kuwa barabara zitakazofungwa zitahusisha zile
za Kata ambazo zitakuwa zinahudumiwa na Ofisi za kata ili kuwawezesha wananchi
kufanya biashara kwa uhuru na kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo yao.
OMBAOMBA.
Kuhusu ombaomba
amesema kuwa mkoa wake utalishughulikia kwa nama ya kipekee kwa kuwa kumekuwa
na ongezeko la ombaomba ambao wamegawanyika katika makundi ya watu wazima na watoto ambao sasa wamekuwa kero kwa
wakihusishwa na vitendo vya ukwapuaji wa mali za watu, kuharibu magari pindi
wanapokosa fedha walizoomba kutoka kwa watumia barabara.
Amewaagiza
wenyeviti wa Kamati za ulinzi na Usalama wa mkoa huo katika kila wilaya kulifanyanyia
kazi suala hilo wakishirikiana na maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha hakuna
watoto wanaozunguka kuombaomba kwa kuwa walitakiwa kuwa shule na elimu sasa
inatolewa bure.
KERO YA USAFIRI.
Amepongeza
juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Mradi wa Mabasi ya mwendokasi ambayo
yamekuwa msaada kwa wakazi wa jiji hilo pia uwepo wa Treni za abiria za reli ya
Kati katika jiji la Dar es salaam kutokea Dar es salaam stesheni hadi Ubungo na
Pugu.
Aidha, mkoa
umeiomba Wizara ya Ujenzi, Mawasliano na Uchukuzi kuangalia uwezekano wa
kuanzisha boti tatu za kisasa zitakazoanzia safari yake Feri kwenda Mtoni Kijichi
na Mbagala na wataalam wa wizara husika wanafanya upembuzi yakinifu kuwezesha
jambo hilo wakati ukisubiriwa utekelezaji wa Awamu ya pili na tatu wa ujenzi wa
mradi wa mabasi ya mwendokasi katika jiji hilo.
Kuhusu msongamano
wa malori ya mafuta yanayokuja katika Bandari ya Dar es salaam kuchukua mafuta,
mkoa huo kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi pamoja
na Wizara ya Nishati na Madini umeweka mkakati wa kuangalia uwezekano wa
kujenga bomba la mafuta litakalotoka Kurasini hadi chalinze kupitia njia ya mradi
wa Tazama ambalo litapunguza msongamano wa malori yapatayo 1000 hadi 1500 yanayoingia na kutoka katika jiji hilo.
ULINZI NA USALAMA.
Amesema kuwa
Serikali ya mkoa wa Dar es salaam itaendelea kuhakikisha kuwa jiji la Dar es
salaam linakuwa salama na kuvitaka vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa Jeshi la
Polisi kuendelea kutekeleza sheria na majukumu yao ipasavyo ili kudhibiti
vitendo vya kiharifu na uvunjaji wa sheria, ujambazi, umiliki silaha haramu,
madawa ya kulevya, vitendo vya udharirishaji wa binadamu .
“Kipindi cha
nyuma silaha zilikua zinalia hovyo sasa nalishukuru Jeshi la Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es salaam kwa kazi nzuri, tutaendelea kuhakikisha ulinzi na
usalama unakuwepo kwa kufanya oparesheni za wamiliki silaha kinyume cha sheria
kuondoa kila aina ya uharifu unaofanyika ndani ya majumba ya watu katika jiji
hili” Amesisitiza Mhe. Makonda.
No comments:
Post a Comment