Waziri wa Nchi
ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akizungumza wakati
wa uzinduzi wa warsha ya kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya
maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeratibiwa
na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha ya
kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa
umma nchini leo Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeratibiwa na Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma.Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais
Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki na Profesa John Kessy kutoka Chuo
Kikuu cha Kilimo (SUA) ambaye ndiye aliyefanikisha utafiti huo.Katibu wa Maadili ya Viongozi – Siasa, Waziri Kipacha akielezea jambo wakati wa warsha ya kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeratibiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.Kutoka kulia ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki na Profesa John Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) ambaye ndiye aliyefanikisha utafiti huo.
Profesa John Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) akiwasilisha rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma katika warsha iliyoandaliwa na Sekrtetarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki (wapili kutoka kulia) na Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda (kushoto) wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini katika warsha warsha ya kujadili rasimu hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujadili Taarifa ya rasimu ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Phillip Mangula akiteta jambo na Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Twaha Taslima walipokuta katika warsha ya kujadili Taarifa ya rasimu ya Utafiti
kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi ofisi
ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa Dini pamoja na Vyama vya Siasa nchini mara baada ya uzinduzi wa warsha ya kujadili
rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini
leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi
– CUF Twaha Tasrima, : Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Jaji Mstaafu Salome Kaganda, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Phillip Mangula. Picha na Frank Shija,
Maelezo)
No comments:
Post a Comment