TANGAZO


Sunday, August 28, 2016

Raia zaidi kuondolewa katika mji wa Darayya Syria

Darayya Syria

Image captionDarayya Syria
Raia zaidi wanatarajiwa kuondolewa kutoka mji unaodhibitiwa na waasi wa Darayya ulio kwenye vitongoji vya mji mkuu wa Syria Damascus hii leo.
Watu hao wanapelekwa kwenye makao yaliyo maeneo yanayodhibitiwa na serikali.
Mwandishi wa BBC eneo hilo anasema kwa kuna wasiwasi kwamba raia walioshirika maandamano ya kuipinga serikali ya rais Assad huenda wakateswa.
Umoja wa mataifa unasema kuwa kuhamishwa kwa raia hao kunastahili kuwa kwa hiari.

No comments:

Post a Comment