TANGAZO


Monday, August 8, 2016

MAADHIMISHO YA MIAKA 80 YA SIMBA 'SIMBA DAY' AFC LEOPARDS YAPIGWA 4-0 UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM

(Picha zote na Habari/Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
TIMU ya Simba ya jijini Dar es Salaam Tanzania, leo imeadhimisha miaka 80 tokea kuanzishwa kwake kwa kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo usafi wa mazingira, kuwaona wagonjwa mahospitalini na mambo mengine kadhaa.

Katika maadhimisho hayo ambayo pia hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa msimu na kujulikana kwa jina la Simba Day maadhimisho hayo hufanyika Uwanja wa Taifa jijini na kwa siku ya leo kulikuwa na shughuli mbalimbali za michezo pamoja na burudani za ngoma na michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi, michezo ya kuigiza na mengineyo.

Pia wachezaji wa siku nyingi wa klabu hiyo, hutoana jashowenyewe kwa wenyewe ama kualikwa timu za vilabu vingine kupambana nazo.

Katika mchezo mkuu wa kuipima timu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu kwa mwaka 2016, Kikosi kipya cha Simba kilichosajiliwa kwa ajili ya ligi hiyo, leo kimepambana na timu ya nchi jirani ya Kenya, AFC Leopards na kukubali kichapo cha mabao 4-0, huku wachezaji wapya wa kikosi cha Simba wakionesha cheche zao kwamba mara hii wamedhamiria kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom. 

Alikuwa ni mchezaji mwenye kasi na chenga za maudhi wa kikosi hicho, Ibrahim Ajibu aliyeanza kuwatia machungu wageni hao, waliokuwa wakionesha kandanda safi kipindi cha kwanza kwa kulishambulia lango la Simba mara kwa mara lakini wakajikuta kijana huyo, akiwatungika bao la kwanza kwa shuti la kuunganisha.

Kipindi cha kwanza kilimalizika Simba ikiwa mbele kwa bao hilo, lililodumu kwa muda wote wa kipindi hicho baada ya kufunga kwenye muda wa dakika 35 za mchezo huo.

Kipindi cha pili Simba waliwatoa baadhi ya wachezaji wao walioanza kwenye kipindi cha kwanza na kuwaingiza wapya walioliandama lango la wageni hao na Ibrahim Ajibu akangeza lingine baada ya kumegewa pande na mchezaji mpya aliyekuwa akiwasumbua Simba kwa muda mrefu katika kuipata saini yake, Laudit Mavugo kutoka Rwanda.

Simba waliendelea kulisumbua lango la wapinzani wao hao kwa kasi na chenga za maudhi na kisha kubahatika kufunga bao la tatu lililowekwa kimiani na mchezaji mpya wa timu hiyo, Shiza Kichuya kwenye dakika ya 70 ya mchezo huo.

Simba hawakuishia hapo, waliendelea kulisumbua lango la wageni wao hao, huku foadi yao ikiongozwa na Laudit Mavugo aliyeonekana mwiba wa kuotea mbali na kwenye dakika ya 80 mchezaji huyo akaiandikia timu yake hiyo bao la nne na la mwisho katika mchezo huo, uliokuwa wa vuta nikuvute na hivyo kuwasisimua na kuwatia kiwewe mashabiki wa timu hiyo waliofurika uwanjani hapo.
Mashabiki wa simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao dhidi ya AFC Leopards ya Kenya Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezaji Shiza Kichuya wa Simba akijaribu kumtoka Cresten Mwanzo wa AFC Leopards ya Kenya. 
Frederic Blagnon wa Simba akijaribu kumpiga chenga golikipa wa AFC Leopards Ian Otieno.
Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo, lililofungwa na Ibrahim Ajibu. 
 Ubao wa matokeo ukionesha Simba bao 1 na AFC Leopards 0.
Hapa mmoja wa wazee na aliyekuwa mchezaji wa Simba, Khamis Kilomoni, akikata keki ya kuadhimisha miaka 80 ya timu hiyo, wakati wa mapumziko ya mchezo huo.
Mzee Khamis Kilomoni, akiendelea kukata keki ya kuadhimisha miaka 80 ya timu hiyo, wakati wa mapumziko ya mchezo huo. 
Mzee Khamis Kilomoni, akiwalisha keki hiyo, vijana wawili. 
Mzee Khamis Kilomoni, akiwalisha keki hiyo, vijana wawili. 
Mzee Khamis Kilomoni, akimlisha keki hiyo, Rais wa Klabu hiyo, Aveva.
Mzee Kilomoni, akimlisha Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Godfrey Nyange Kaburu.
Mzee Kilomoni, akimlisha keki Naibu Waziri wa Afya na mwanachama wa Simba, Dk. Khamis Kigwangalla.
Mzee Kilomoni, akimlisha keki mwanachama wa Simba, Athuman Kapuya huku akisaidiwa na mwanachama mwenzake, Mohamed Dewj.


Mzee Kilomoni, akimlisha keki mwanachama wa Simba, Mohamed Dewj.
Mzee Kilomoni, akimlisha keki Alex Karia.
Mzee Kilomoni, akimlisha keki mmoja wa wanachama wa Simba.
Mwanachama wa Simba, Mohamed Dewj, ambaye anategemewa kumiliki hisa 51 az klabu hiyo, akimlisha keki mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mwanachama wa Simba, Mohamed Dewj, ambaye anategemewa kumiliki hisa 51 az klabu hiyo, akimlisha keki mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mzee Kilomoni akimlisha keki mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa timu hiyo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa timu hiyo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa timu hiyo. Kushoto ni mwanachama wa klabu hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Khamis Kigwangala na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EGT, Iman Kajula, waratibu wa biashara za Simba.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia mpira wakati kiliponza kipindi cha pili. 
Mchezaji Edwin Wafula wa AFC Leopards akipambana na Ibrahim Ajibu wa Simba.
Mchezaji Benard Ongoma wa AFC Leopards akipambana na Ibrahim Ajibu wa Simba.
Mchezaji Benard Ongoma wa AFC Leopards akipambana na Ibrahim Ajibu wa Simba.
Mchezaji Benard Ongoma wa AFC Leopards akipambana na Ibrahim Ajibu wa Simba katika mchezo huo.
Mchezaji Ibrahim Ajibu wa Simba, akiwa amedondoka chini.
Wachezaji wa Simba, wakishangilia kwa kuswali, bao la pili lililofungwa na Ibrahim Ajibu.
Wachezaji wa Simba, wakishangilia kwa kuswali, bao la pili lililofungwa na Ibrahim Ajibu.
Wachezaji wa Simba, wakishangilia kwa kuswali, bao la pili lililofungwa na Ibrahim Ajibu.
Ubao wa matokeo ukionesha Simba mabao 2 na AFC Leopards 0.
Jamal Mnyate wa Simba akipambana na mchezaji wa AFC Leopards.
Ibrahim Ajibu akimpongeza Laudit Mavugo kwa kumpatia pasi aliyoifungia Simba bao la pili.
Wachezaji wa Simba, wakishangilia bao la tatu la timu hiyo, lililofungwa na Shiza Kichuya
Ubao ukionesha Simba mabao 3 na AFC Leopards 0.
Laudit Mavugo akishangilia bao la nne aliloifungia timu yake ya Simba.
Na mwisho ubao wa matangazo ukionesha Simba mabao 4 na AFC Leopard 0.

No comments:

Post a Comment