KATIKA kufanikisha agizo la mhe. Rais John Magufuli, na kutekeleza maamuzi ya kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Dodoma, tbc imeamua kuandaa kipindi maalum ili kuwafahamisha wananchi juu ya uamuzi huo, faida zake na pia nini kifanyike au nini kimefanyika mpaka sasa. Kipindi hiki kinaitwa “SAFARI YA DODOMA” ambacho kinarushwa kila siku ya jumatano saa 3:00 usiku, TBC1.
Kipindi hiki cha muda wa saa moja, kinawakaribisha wadau mbalimbali toka serikalini, mashirika na jamii kupata fursa kuja kuelezea umuhimu na jinsi ambavyo wamejiandaa kuhamia Dodoma, pia ni fursa gani zilizopo Dodoma, zikiwemo jitihada za wafanyabiashara na wawekezaji kutumia nafasi hii kuelezea namna ambavyo wanaweza kustawisha makao makuu ya nchi, Dodoma.
Kipindi cha kwanza kilichorushwa jumatano iliyopita ya tarehe 10 agosti 2016, tulikuwa na mhe. Cleopa Msuya, waziri mkuu mstaafu. Ambaye alitueleza hali ilivyokuwa wakati huo ameteuliwa kuwa waziri mkuu, na jinsi ambavyo maamuzi ya kuhamia Dodoma yalitekelezwa.
Katika kipindi cha jumatano tarehe 17 Agosti 2016, saa 3:00 usiku, kwenye studio za TBC1 tutakuwa na mgeni, mhe. Jenister Mhagama, waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge, kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu.
Pia tutakuwa na nafasi ya kuwasikiliza wadau mbalimbali wakitoa maoni yao kuhusiana na maamuzi haya, pia tutakaribisha simu ili kujibu maswali mbalimbali yatakayotolewa kwenye kipindi, ambapo mshindi atajipatia zawadi toka chuo kikuu cha Dodoma (udom).
Nakukaribisha kutazama kipindi hiki, jumatano saa 3 usiku, TBC1
Kwa maoni tutumie barua pepe: maonidodoma@tbc.go.tz
Pia jiunge nasi katika mitandao ya kijamii:
SMS: Andika dodoma, acha nafasi, Ujumbe wako, tuma kwenda 15559
WhatsApp: 0678 279 107
Facebook: tbconetanzania
Twitter: tbconetanzania
Instagram: tbconetanzania
Youtube: TBC1
No comments:
Post a Comment