TANGAZO


Thursday, August 25, 2016

Kiongozi wa Brexit Nigel Farage ahutubu mkutano wa Donald Trump

Donald Trump and Nigel Farage

Image copyrightAP AND AFP
Image captionBw Farage amesema angekuwa Mmarekani hawezi kumpigia kura Bi Clinton hata akilipwa

Mwanasiasa mmoja wa Uingereza aliyeongoza kampeni ya kujiondoa kutoka ndani ya Umoja wa Ulaya (EU), Nigel Farage, amehutubia mkutano mmoja wa kampeni za urais wa chama cha Republican nchini Marekani.
Huku mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump akisimama sako kwa bako naye, kinara huyo anayeondoka wa chama cha UK Independence Party (UKIP), amewaambia wafuasi wa Republican kuwa mambo mengi yanawezekana watu wema wakisimama kidete kupinga uongozi wowote ule.
Mkutano huo uliofanyika Jackson, Mississippi umehudhuriwa na jumla ya wanaharakati 15,000 wa chama cha Republican.
Wakati wa kampeni ya kutetea kujiondoa kwa UIngereza kutoka EU, Bw Trump alitangaza uungaji mkono wake.
Bw Farage, akihutubu, amesema kampeni inayoendeshwa kwa sasa na chama cha Republican inatoa "fursa nzuri sana".
"Mnaweza kuwashinda watu wanaofanya kura za maoni, mnaweza kuwashinda wachanganuzi wa masuala ya kisiasa na kiuchumi, mnaweza kuwashinda watu wanaodhibiti Washington," amesema.
Kiongozi huyo wa UKIP pia alihudhuria mkutano mkuu wa kuidhinisha mmgombea urais wa Republican jijini Cleveland, hio mwezi uliopita.

Nigel FarageImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionBw Nigel Farage

Alikuwa amedokeza wakati huo kwamba angekuwa makini na kwamba hangeingia kwenye mtego wa kumuidhinisha, binafsi, Bw Trump.
Lakini akihutubu Mississippi, amesema iwapo angelikuwa mpiga kura wa Marekani, hawezi kumpigia kura mpinzani mkuu wa Bw Trump, Bi Hillary Clinton wa chama cha Democratic, hata akilipwa.
Bw Trump, akihutubu katika mkutano huo, amemsifu Nigel Farage na kusema aliwezesha Uingereza kuchukua tena udhibiti wa mipaka yake - wakati wa kura ya kujiondoa kutoka EU.

No comments:

Post a Comment