TANGAZO


Monday, August 15, 2016

JAJI LUBUVA AMTEMBELEA SPIKA NDUGAI, AMKABIDHI RIPOTI YA UCHAGUZI WA MWAKA 2015

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva  (kulia), akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benjamin Sawe-Maelezo)
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam. 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.  
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 wakati alipokwenda kumtembelea nyumbani kwake Salasala Jijini Dar es Salaam.

By Christina Njovu
Mwenyekiti wa Tume ya Taifaya UchaguziJajiMstaafu Damian Lubuva leo amemtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Job Ndugai nyumbani kwake Jijini Dar es Salam na kumjulia hali baada ya kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu.

Akiwa nyumbani kwa spika Jaji Lubuva pia amemkabidhi Mh.Ndugai ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015 na kumueleza kuwa kukamilika kwa ripoti hiyo, ndio hitimisho la Uchaguzi Mkuu na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao.

Kwa upande wake Mheshimiwa Ndugai ameipongeza hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya kuweka mikakati ya kushiriki katika maonyesho mbalimbali yakiwemo yale ya biashara ya Saba Saba na Nane nane katika kutoa elimu kwa wananchi.


Jaji Mstaafu Lubuva alikwenda kumjulia hali Ndugai ambaye kipindi cha Bunge la Bajeti lililomalizika hivi karibuni, alikuwa nchini India kwa matibabu na hivi sasa afya yake imezidi kuimarika.

No comments:

Post a Comment