TANGAZO


Monday, August 15, 2016

HASSAN ABBAS: UJIO WA MUIGIZAJI LUCY UWE CHACHU KWA MAENDELEO YA SANAA NCHINI


Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bw. Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya uzinduzi wa igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa)  jana Agosti 14, 2016. (Picha zote na Raymond Mushumbusi Maelezo)
Msanii mkongwe nchini Ahmed Olutu (Mzee Chilo) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya uzinduzi wa igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa)   jana Agosti 14,2016. 
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Bw. Hassan Abbas akijadiliana jambo na Msanii wa Bongo Movie Single Mtambalike(Richie Richie) wakati wa uzinduzi wa igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa)  katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jana Agosti 14,2016.
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo, Bw. Hassan Abbas(wa pili kulia) akifatilia igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa)  wakati wa uzinduzi wa igizo hilo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jana Agosti 14,2016.  

Juu na chini: Baadhi ya matukio katika igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa), likiwa limeigizwa na Msanii kutoka Marekani Bi Toussaint Duchess kwa kushirikiana na wasanii kutoka Tanzania kama vile Yvonne Cherly  (Monalisa) na  Suzan Lewis(Natasha) lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jana Agosti 14,2016.



Juu na chini: Baadhi ya matukio katika igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa), likiwa limeigizwa na Msanii kutoka Marekani Bi Toussaint Duchess kwa kushirikiana na wasanii kutoka Tanzania kama vile Yvonne Cherly  (Monalisa) na  Suzan Lewis(Natasha) lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jana Agosti 14,2016. 

Juu na chini: Baadhi ya matukio katika igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa), likiwa limeigizwa na Msanii kutoka Marekani Bi Toussaint Duchess kwa kushirikiana na wasanii kutoka Tanzania kama vile Yvonne Cherly  (Monalisa) na  Suzan Lewis(Natasha) lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jana Agosti 14,2016. 

Baadhi ya matukio katika igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika(Mrs. Lucy goes to Africa)  likiwa limeigizwa na Msanii kutoka Marekani Bi Toussaint Duchess kwa kushirikiana na wasanii kutoka Tanzania kama vile Yvonne Cherly  (Monalisa) na  Suzan Lewis(Natasha) lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jana Agosti 14,2016. 
Baadhi ya wageni waalikwa na mashabiki waliohudhuria igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa), wakifuatilia igizo hilo lililofanyika jana katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Agosti 14,2016 jijini Dar es Salaam. 
Juu na chini: Msanii kutoka Marekani Bi Toussaint Duchess (Mama Lucy), akiwashukuru wageni waalikwa na mashabiki mara baada ya kumalizika kwa igizo lake la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa) lililofanyika jana katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Agosti 14,2016. 

Msanii kutoka Marekani Bi Toussaint Duchess (Mama Lucy), akiwashukuru wageni waalikwa na mashabiki mara baada ya kumalizika kwa igizo lake la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa) lililofanyika jana katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Agosti 14,2016. 

Na Immaculate Makilika- Maelezo
MKURUGENZI wa Idara ya habari (Maelezo), Bw. Hassan Abbas amesema kuwa ujio wa msanii wa maigizo kutoka nchini Marekani Bi. Toussaint Duchess maarufu kama Mama Lucy uwe changamoto kwa wadau wa sanaa nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mheshimiwa Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi  kwenye  uzinduzi wa igizo la   msanii Lucy linaloitwa Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa)  mwishoni mwa wiki Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Abbas alisema kuwa ni vyema  wadau wa sanaa wakatumia ujio huo kama changamoto itakayowasaidia kujifunza na kuwa  wabunifu zaidi katika kazi zao za sanaa.
“Ujio wa muigizaji Lucy ni changamoto kwa wadau wa sanaa nchini, ni fursa ya kujifunza kwa wasanii hususani katika eneo la sanaa za jukwaani, vile vile ni fursa kwa vijana wa kitanzania ambao wanatarajia kufanya kazi  za sanaa” alisisitiza Bw. Abbas
Aliendelea kwa kusema kuwa Serikali inatoa pongezi kwa kituo cha televisheni cha Azam na wasanii mbalimbali wakiwemo Suzan Lewis (Natasha) na Yvone Cherry (Monalisa) ambao wameshiriki  kwa ubunifu wa kumleta msanii huyo nchini pamoja na maboresho mengine yanayofanywa na kituo hicho cha televisheni cha Azam.
Aidha, aliongeza kuwa  akiwa Msemaji wa Serikali, anatarajia kushirikiana  na wadau wa sanaa  nchini kupitia mikakati mbalimbali itakayoandaliwa ili kuunga mkono juhudi aliyoanza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kujali na kusimamia kazi za sanaa na wasanii ili waweze kunufaika na kazi zao.
Kituo cha televisheni cha Azam kinatarajiwa kuonesha igizo hilo la msanii huyo kutoka nchini Marekani liloandaliwa kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali kutoka nchini wakiwemo Suzan Lewis (Natasha) na Yvone Cherry (Monalisa) pamoja na filamu mbalimbali zitakazofanywa na msanii huyo.

No comments:

Post a Comment