TANGAZO


Monday, August 15, 2016

DRC yaomboleza mauaji

Waasi wa ADF


Image captionWaasi wa ADF

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hii leo inaadhimisha siku tatu za maombolezi kufuatia mauaji ya raia 30 siku ya Jumamosi.
Jeshi limelaumu waasi wa ADF kwa vifo hivyo katika kijiji cha Rwangoma karibu na mji wa Beni Kaskazini mwa mkoa wa Kivu.
Raisi kabila akiwa ziarani katika eneo hili la mashariki mwa congo,ametangaza kwenye vyombo vya habari kupitia msemaji wa serekali kwamba, mauaji yanayo tendeka mjini BENI yanapashwa kuchukuliwa kama tishio la kigaidi .
Kabila alisisitiza kwamba  ametowa wito  mara kadhaa katika mikutano ya ICGLR,Amewataka raia wa DRC kushikamana katika siku tatu hizi za maombolezo ambapo bendera ya yaifa inapepea nusu mlingoti.Licha ya serekali kutoa idadi ya 36 mashirika ya kiraia imetangaza hivi punde idadi ya watu 52 na kusema kuna uwezekano wa idadi hiyo kupanda.

Rais Joseph Kabila
Image captionRais Joseph Kabila

Serikali na Umoja wa Mataifa umelilaumu kundi hilo kwa ghasia za kila mara katika eneo hilo.Makumi ya waandamanji walikongamana mjini Beni baada ya shambulio hilo la siku ya Jumamosi.
Wakibeba mmoja wa mwili wa waathiriwa hao ,waliimba nyimbo dhidi ya serikali kulingana na shahidi aliyezungumza na kituo cha habari cha AFP.
Jeshi limelaumu waasi wa ADF kwa vifo hivyo katika kijiji cha Rwangoma karibu na mji wa Beni Kaskazini mwa mkoa wa Kivu.
Serikali na Umoja wa Mataifa umelilaumu kundi hilo kwa ghasia za kila mara katika eneo hilo.
Makumi ya waandamanji walikongamana mjini Beni baada ya shambulio hilo la siku ya Jumamosi.
Wakibeba mmoja wa mwili wa waathiriwa hao ,waliimba nyimbo dhidi ya serikali kulingana na shahidi aliyezungumza na kituo cha habari cha AFP.

No comments:

Post a Comment