Takriban 18,000 wamefariki katika jela za serikali nchini Syria tangu kuanza kwa maandamano dhidi ya serikali mwaka 2011 kulingana na shirika la habari la Amnesty International.
Ripoti mpya ilioandikwa na shirika hilo la hisani, lililowahoji waathiriwa 65,inaelezea utumizi wa ubakaji na kipigo walichopata kutoka kwa walinzi wa jela.
Wafungwa wa zamani walielezea sherehe za kukaribishwa katika jela kupitia tambiko la kupigwa kwa kutumia vyuma na nyaya za stima.
Serikali ya Syria kwa mara kadhaa imekana madai hayo.
Ripoti hiyo inakadiria kwamba takriban watu 17,723 walifariki wakiwa kizuizini kati ya mwezi Machi mwaka 2011 wakati maandamano hayo dhidi ya rais Bashar Assad yalipoanza na Disemba 2015 sawa sawa na takriban watu 10 kila siku ama zaidi ya watu 300 kwa mwezi.
Kulingana na ripoti hiyo ,wafungwa wapya hufanyiwa ukaguzi wa kiuasalama ambao unahusisha wanawake wanaohusishwa kingono na walinzi wa kiume.
No comments:
Post a Comment