Mwanamuziki chipukizi kutoka Gabon amefurahi sana baada ya mwanamuziki nyota wa ''Bluez'' kutoka Canada Celine Dion kusambaza video yake akiimba moja ya vibao vyake.
Samuel mwenye umri wa miaka 17 alijirekodi akiimba wimbo wa ''The Power of Love'' akiwa Libreville.
Video hiyo imetazamwa na mamilioni ya watu kwenye mtandao wa Facebook.
Hata hivyo Samuel alihisi yuko kwenye wingu la tisa Mwimbaji huyo nyota aliposambaza video hiyo na kuandika ujumbe wa kumtia shime kuwa
''Samuel talanta yako ni ya kuvutia sawa na sauti yako''
''Natamani kukutana nawe siku moja''
Wimbo huo ambao ulitungwa na Jennifer Rush, uliuzwa na kupata umaarufu mkubwa mwaka wa 1993 ulipopigwa upya na bi Dion.
Celine aliendelea kusema kuwa amefurahi kuwa wimbo wake umewavutia mashabiki kote duniani.
Samuel aliiambia shirika la habari la AFP kuwa amepigwa na butwaa kuwa talanta yake imemvutia Celine Dion.
''Kwa hakika sikutarajia hilo lingewahi kutokea.
''kwa sasa sina simu wala anuani ya mtandao wa facebook kwa hivyo kakangu aliponieleza kuwa Celine Dion alikuwa ametambua kipaji changu, nilifurahi sana''
''Natumai siku moja itafika nitakapokutana naye uso kwa uso''
''Tayari watayarishi wa mashindano ya muziki wamenitafuta kwa nia ya kunisajili sio tu Ivory Coast bali hata Ufarasansa.
''Kwa hakika sijazoea umaarufu wa aina hii''
Hata hivyo majuzi alipokuwa akiimba wakati wa likizo alipigwa na butwaa wanafunzi wenzake walipompigia makofi alipoingia darasani wengi wakishangaa kuwa anauwezo na kipaji kama hicho cha uimbaji''
Samuel amesema kuwa anatarajia kunoa kipaji chake kimuziki na huenda akaamua kuwa mwanamuziki.
No comments:
Post a Comment