Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi. Kusoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Nyamagori Omari.
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw.
Kassian Chibogoyo (katikati) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani), baadhi ya vielelezo sahihi vya
Taifa vinavyotakiwa kutumiwa na wananchi wakati alipokuwa akielezea umuhimu wa
wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa na kuachana na vile vya kughushi
mapema leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari
(Maelezo) Bw. Frank Shija na kushoto ni Afisa Habari toka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Nyamagori Omari.(Picha zote na Eliphace Marwa -
Maelezo)
Na
Frank Shija, MAELEZO
KATIKA kuhakikisha heshima, hadhi na maadili miongoni mwa jamii ya Watanzania
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais John Pombe Magufuli
imewakumbusha wananchi kuheshimu na
kuzingatia matumizi sahihi ya Vielelezo vya Taifa.
Haya
yamebainishwa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Cassian Chibogoyo alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari katika Kipindi chake cha ‘Tujikumbushe’’
Sehemu ya Pili kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Chibogoyo
amesema amesema kuwa wakati sasa umefika kwa jamii kuendeleza utamaduni
uliokuwapo wa kuheshimu na kufuata desturi zilizowekwa katika kuendeleza umoja,
amani na mshikamano.
‘Natoa
wito kwa watanzania wote, katika kufanya maboresho ya kurejesha hadhi ya taifa
tunapaswa kuheshimu sana Vielelezo vya Taifa letu, hapa na maanisha tuheshimu
wimbo wa taifa na Nembo ya Taifa.’
Amesema
kuwa katika kuhakikisha vielelezo hivyo vinaheshimiwa Ofisi yake imejipanga
kufuatilia kwa karibu wale wote watakao kiuka matumizi sahihi ya Vielelezo vya
Taifa ikiwemo Nembo, Bendera na Wimbo wa Taifa.
Aliongeza
kuwa kuanzia sasa matumizi ya Bendera ya Taifa yatakwenda sambamba na matumizi
ya Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo amezitaka Ofisi zote za
Serikali pamoja na Taasisi zake waanze utaratibu wa kupandisha pia bendera hiyo
kwani Tanzania tunaamini katika ushirikiano huo.
Katika
hatua nyingine uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu (TUGHE) Tawi la
Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali wamekanusha tuhuma zilizoandikwa na moja
ya gazeti hapa nchini(Jina limehifadhiwa) zikimtuhumu Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali kuwa na kusema kuwa tuhuma zilizoandikwa katika Gazeti hilo siyo
zakweli na ata wao kama wafanyakazi wameshangazwa.
Katibu
wa TUGHE Tawi la Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali amesema kuwa ni vyema waandishi
wakafanya kazi zao kwa weledi kuliko kuandika taarifa zizizosahihi kwani
kufanya hivyo kuta waingiza matatizoni.
Nilitegemea
kabla mwandishi hajachapisha habari ile angetafuta ukweli kutoka upande wa pili
ikiwemo kuhusishwa kwa uongozi wa Chama cha Wafanyakazi kwani ndiyo wenye
mamlaka yakutoa taarifa katika ngazi husika kwa tupo kwa ajili ya kuwawakilisha
na kuwatetea wafanyakazi.
Kipindi
cha Tujikumbushe kimekuwa kikionyeshwa na TBC1 ambapo lengo lake kuu ni kutoa
elimu kwa jamiii juu ya matumizi sahihi na umuhimu wa kutunza nyaraka na tunu
za Taifa, ambapo Sehemu ya Kwanza ya kipindi hicho kilihusu Nyaraka za
Serikali. Kipindi kinachofuata kitahusu Historia ya kuwepo kwa Katiba na Katiba
inayopendekezwa.




No comments:
Post a Comment