Pages

Tuesday, June 28, 2016

Wimbo wa matusi wamtia 50 Cent matatani Caribbean


Image copyrightGETTY
Image captionWimbo wa matusi wamtia 50 matatani Caribbean

Mwanamuziki wa kufoka kutoka Marekani 50Cent alilazimika kulipa faini ya dola elfu ishirini pesa za Marekani baada ya kutumia maneno yenye matusi alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko katika kisiwa cha St Kitts and Nevis.
Fifty cent ambaye anafahamika kwa jina kamili Curtis Jackson alikuwa amepangiwa kuwa 'Mcee' katika tamasha hilo la muziki huko Caribbean lakini alipopanda jukwaani mashabiki walimsihi awape kionjo cha muziki wake.

Image copyrightGETTY
Image captionFifty cent anafahamika kwa jina kamili Curtis Jackson

Alipokubali 'DJ' alicheza wimbo wake mmoja na wimbo huo ulikuwa na matusi kochokocho jambo ambalo ni hatia katika kisiwa hicho kilichotawaliwa na Uingereza.
50 cent hakufahamu alikuwa amevunja sheria hadi alipofika katika uwanja wa ndege siku ya Jumapili akikusudia kuondoka.
Hata hivyo maafisa wa forodhani walimkamata na kumzuilia hadi jumatatu alipofikishwa mbele ya hakimu na kusomewa mashtaka yake.

Image copyrightAP
Image caption50 cent alikiri makosa yake na kupigwa faini ya takriban dola 20,000

50 cent alikiri makosa yake na kupigwa faini ya takriban dola 20,000 pesa za marekani kabla ya kuruhusiwa kuondoka.

No comments:

Post a Comment