Pages

Tuesday, June 7, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akiteta jambo na Waziri Mkuu Majaliwa K. Majaliwa, wa Uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 hadi 2020/21, utakaogharimu shilingi Trilioni 107, katika Ukumbi wa Chuo Cha Mipango Dodoma, Juni 7,2016. 
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa K. Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kuzindua Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17/2020/21, utakao gharimu shilingi Trilioni 107,  katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma, Juni 7, 2016. 
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa K. Majaliwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), wakiangalia kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano, wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 hadi 2020/21, utakao gharimu shilingi Trilioni 107, katika Ukumbi wa Chuo Cha Mipango Dodoma, Juni 7,2016. 
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa K. Majaliwa akimkabidhi Naibu Spika Tulia Akson kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano, wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 hadi 2020/21, utakao gharimu shilingi Trilioni 107, katika Ukumbi wa Chuo Cha Mipango Dodoma, Juni 7,2016. 
 
Na Jonas Kamaleki, Maelezo, Dodoma
7.6.2016
UCHUMI wa Tanzania unazidi kukua kwa kiwango cha asilimia 7 kwa mwaka kutokana na juhudi za makusudi zilizofanywa na Serikali ikiwemo kuimarisha miondombinu, ukuzaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano na uchimbaji wa madini.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati alipokuwa akizindua Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/2017- 2020/2021.

Majaliwa alisema Mpango huo unalenga kuboresha maisha ya Watanzania kijamii na kiuchumi ili kuwaondolea umaskini kwa kuweza mkazo katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na viwanda. 

“Umaskini umepungua kwa asilimia 6.2 na bado tunaendelea kufanya juhudi kubwa ili kupunguza umaskini,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza kuwa watanzania 10.78 milioni bado ni maskini.

Kwa mujibu wa Majaliwa alisema kuwa ukuaji wa uchumi inabidi uwe shirikishi kwa kila mwananchi kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali. 

Akizungumzia suala la uwekezaji katika viwanda, Majaliwa alisema Watanzania wanapaswa kuwezeshwa katika kupata mitaji ya kuwekeza na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na  Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema wakati umefika wa kuhakikisha ukuaji wa uchumi unatiliwa mkazo na serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hasa katika viwanda na madini.

“Tumeamua kuboresha miundombinu ikiwemo ya ujenzi wa reli, kuboresha bandari zetu na kufufua Shirika la Ndege (ATCL) na kutekeleza miradi mikubwa ya uchimbaji wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga ambavyo vitaongeza pato la mtanzania kutoka dola za Kimarekani 1006 hadi 1500 ifikapo 2020,” amesema Dkt. Mpango.

Mpango huu wa Maendeleo ambao umezinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu una Kauli Mbiu isemayo “Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kuchochea Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya Watu”.

SERIKALI KUAJIRI WALIMU 35411 KATIKA MWAKA WA FEDHA 2016/17

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Jonas Kamaleki, Maelezo, Dodoma
SERIKALI katika mwaka wa fedha 2016/2017 inatarajia  kuajiri walimu 35,411 katika shule za msingi na sekondari ili kuongeza tija katika sekta ya elimu nchini.

Hatua hiyo ni mkakati wa Serikali wa kukabiliana na upungufu  wa walimu 22,460 wa masomo ya Sayansi na Hisabati katika shule za sekondari, hatua inayoelezwa  kuwafanya wanafunzi kutofanya vizuri katika masomo hayo.

Hayo yamesemwa jana Bungeni na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Buyugu Kasuku Samson Bilago  aliyetaka kujua idadi ya walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati wanaohitajika ili kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.

Profesa Ndalichako ameongeza kuwa idadi ya walimu wa sekondari waliopo kwa sasa ni 88, 999 kati ya hao walimu 18, 545 ni wa masomo ya Sayansi na Hisabati ambapo 70, 454 ni wa masomo ya Lugha, Sanaa na Biashara.

Kuhusu uboreshaji wa miundombinu mashuleni Profesa Ndalichako amesema Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji imeendelea kutenga fedha katika bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mashuleni, ujenzi wa nyumba za walimu, vyoo vya walimu na wanafunzi na ujenzi wa madarasa.

Aidha, Profesa Ndalichako amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 serikali ilitenga bilioni 67.83 ambazo zimeshapokelewa katika Halmashauri mbali mbali na zimetumika kwa ajili ya ukarabati, ujenzi na umaliziaji wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa vyoo na uwekaji wa umeme katika shule za sekondari 528 nchini.

No comments:

Post a Comment