Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (katikati), akiwaonesha waandishi wa habari waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere tuzo na cheti vya tuzo za Ulaya kwenye Ufanisi Bora kwa mwaka 2016, zilizotolewa jijini Brussels nchini Ubelgiji mwishoni mwa wiki iliyopita. Kushoto ni mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Habari la Taifa (TBC), ambao ni wabia na kampuni hiyo, Injinia Diotrefu Abenego ambaye naye pia aliambatana naye kwenye safari hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao, akiwaonesha waandishi wa habari waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere tuzo na cheti vya tuzo za Ulaya kwenye Ufanisi Bora kwa mwaka 2016, zilizotolewa jijini Brussels nchini Ubelgiji mwishoni mwa wiki iliyopita.
Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (kulia), akiwa na tuzo huku Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Habari la Taifa (TBC), ambao ni wabia na kampuni hiyo, Injinia Diotrefu Abenego, akiwa ameshikilia cheti, vilivyotolewa katika tuzo za Ulaya kwenye Ufanisi Bora kwa mwaka 2016, jijini Brussels nchini Ubelgiji mwishoni mwa wiki iliyopita.
Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere, Dar es Salaam, wakati alipowasili na tuzo hiyo. Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao, akionesha tuzo na cheti iliyotunukiwa Kampuni ya StarTimes katika tuzo za Ulaya kwenye Ufanisi Bora kwa mwaka 2016, jijini Brussels nchini Ubelgiji mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere, Dar es Salaam hivi karibuni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao, akionesha tuzo na cheti iliyotunukiwa Kampuni ya StarTimes katika tuzo za Ulaya kwenye Ufanisi Bora kwa mwaka 2016, jijini Brussels nchini Ubelgiji mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere, Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia anayemsaidia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Habari la Taifa (TBC), ambao ni wabia wa kampuni hiyo, Injinia Diotrefu Abenego.
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Juni 7, 2016.
TAASISI ya European Society for Quality Research (ESQR) yenye makao yake makuu jijini Lausanne, Uswizi imeitunuku Tuzo ya Ulaya kwa Ufanisi Bora kampuni ya matangazo ya dijitali ya StarTimes Tanzania mwishoni mwa wiki hii jijini Brussels, Ubelgiji.
Akizungumza na waandishi mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere juu ya tuzo hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao amebainisha kuwa ni furaha kubwa kutambua kwamba kuna watu wanafuatilia utendaji na ufanisi wa shughuli zetu katika kuwahudumia watanzania.
“Leo ninayo furaha kubwa kuwafahamisa wateja wetu na watanzania kwa ujumla juu ya kampuni ya StarTimes kutunikiwa tuzo ya ufanisi bora iliyotolewa barani Ulaya. Kampuni yetu ndiyo ya pekee iliyoshinda tuzo hiyo kwa ukanda wa Afrika ya Mashariki kutokana na mchango wake mkubwa katika utoaji wa huduma za matangazo ya dijitali. Hii ni heshima kubwa kwa StarTimes kwa mchango wake katika kufanya maisha ya watanzania kuwa bora na pia tumeipeperusha vema bendera ya Tanzania kimataifa.” Alisema Bw. Liao
“Kutunikiwa kwa tunzo hii kunamaanisha kwamba taasisi zingine zinatambua mchango tulio nao katika kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na huduma bora za matangazo ya dijitali kwa gharama nafuu inayoweza kumudiwa na kila mtu. Lakini leo tusingeweza kuwa hapa bila ya nguvu na ari kubwa tunayoipata kutoka kwa wateja wetu ambao wanatuunga mkono kwa huduma zetu. Ningependa kusema kuwa tunawashukuru sana kwani tunzo imetokana na kuwahudumia wao kwa ubora na ufanisi mkubwa.” Aliongezea Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo ya matangazo ya dijitali
“Mbali na kuwashukuru wateja lakini pia pongezi za dhati ziiendee serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri kwa wakezaji nchini. Kama mnavyojua kampuni yetu inafanya kazi ikiwa ni ubia pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Hivyo kufanikiwa kwetu pia ni matokeo ya uhusiano mzuri tuliokuwa wao nao. StarTimes tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi na nafuu ili kila mtanzania afikiwe popote alipo, natumaini watanzania wanafurahia maudhui mazuri tunayowapatia kwa sasa na tutazidi kuwaboreshea zaidi.” Alihitimisha Bw. Liao
Naye kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Injinia Diotrefu Abenego ambaye naye alikuwepo kwenye utoaji wa tuzo hizo ameongezea kwa kusema kuwa, “Tuzo hizi zilitolewa kwa makampuni madogo, ya kati na makubwa ikiangazia ubora wa huduma na bidhaa zake, uvumbuzi na ubunifu wa utoaji wa huduma zake kwa wateja wao. Kulikuwa na makampuni 76 kutoka nchi 63 duniani kote yakifanya shughuli mbalimbali kama vile sekta za Elimu, Afya, Kilimo na kadhalika. Kwa upande wa Afrika ya Mashariki StarTimes Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Star Media Afrika ndiyo iliiwakilisha nchi yetu, na kama mjuavyo StarTimes inafanya kazi kwa ubia na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Hivyo ni heshima kubwa kwetu na pia chachu kwa makampuni ya ndani kufanya vema kimataifa, kwa mfano nchi ya Ghana ilipokea tuzo nyingi.”
Tunzo ya Ulaya kwa Ufanisi Bora hutambua taasisi, makampuni, mashirika binafsi na ya umma pamoja na watu binafsi wenye kujitolea kwa namna yake na kuleta matokeo mazuri kwenye mikakati ya uboreshaji wa ubora.
Mbali na kampuni ya StarTimes, makampuni mengine yaliyowahi kupokea tunzo hii ni pamoja na Phillips ya Uholanzi (2012), Konica Minola ya Japan (2015), Carlsberg Breweries ya Denmark (2013), All Nipon Airways ya Japan (2013) na Delta Air Lines ya Marekani (2014).







No comments:
Post a Comment