Mwenyekiti wa Mfuko wa Good Hope Star na Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Albino duniani Al Shamaymaa Kwegyir akifafanua jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari (hawapopichani) leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujulisha umma siku ya maadhimisho ya Albino duniani.Kutoka kuliani Mwenyektiwa TAS Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TAS, Musa Katimba (kushoto) na Mwenyekiti wa TAS Taifa Nemes Temba.
Wandishi wa habari wakichukua
matukio wakati wa mkunano baina ya TAS na waandishi wahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO leo jijini Dar es
Salaam.(Picha zote na Frank Shija, Maelezo)
Na Lilian Lundo, Maelezo
MHE Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino
yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Akiongea
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama cha Watu
Wenye Ualbino Nchini (Tanzania Albinism Society) Nemes Temba ameeleza
kuwa kupitia maadhimisho hayo jamii itapata fursa ya kupewa elimu muhimu kuhusu
ualbino ili kuondoka na dhana potofu hususani ushirikina.
“Maadhimisho
haya ambayo yataanza Juni 11 hadi Juni 13, 2016 yatasindikizwa na mambo
mbalimbali ikiwemo huduma za afya hususani uchunguzi na matibabu ya
saratani ya ngozi pamoja na nasaha za viongozi na mabalozi, utambulisho wa Miss
Albino Tanzania na uzinduzi wa kamusi ya ulemavu,” alisema Temba.
Temba
aliendelea kuainisha kwamba siku hiyo itawapa fursa watoto wenye ualbino
waishio kwenye vituo mbalimbali nchini kutembelea mji wa Bagamoyo kujionea
mambo mbalimbali chini ya ufadhili wa shirika la UNICEF.
Aidha
Mwenyekiti huyo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa
vipaumbele watu wenye ulemavu akiwemo Dkt. Abdallah Possi ambaye ni Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu hii
inadhihirisha kuwa ulemavu si hoja bali utendaji kazi ndio kitu umuhimu.




No comments:
Post a Comment