
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akimshukuru Balozi wa Norway Nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad kutokana na miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo nchi hiyo imekuwa ikiifanya hapa nchini. Mhe. Wambura alikutana na Balozi huyo leo mjini Dodoma. (Picha zote na Anna Nkinda)
Mhe. Balozi wa Norway Nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad (kushoto) akimweleza Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na Norway hapa nchini ukiwemo mradi wa kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia VICOBA.
Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimwonyesha Balozi wa Norway nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad picha za mazao ya mbogamboga ambayo yamelimwa katika kilimo kinachowezesha mazao mchanganyiko kustawi katika mazingira yenye hali ya hewa iliyodhibitiwa mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimpa zawadi ya kanga Balozi wa Norway Nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo mjini Dodoma.
Balozi wa Norway nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad akivaa kanga aliyopewa zawadi na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura aliyekutana naye leo mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Wambura akimwangalia.
Balozi wa Norway nchini Mhe. Hanne – Marie Kaarstad akimshukuru Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura kwa zawadi ya kanga aliyompa.






No comments:
Post a Comment