Pages

Saturday, June 11, 2016

Ibada ya kumkumbuka Ali yajawa na mihemko



Image copyrightAP
Image captionBill Clinton

Ibada ya ukumbusho iliojawa na mihemko ya aina yake kwa bondia Mohammed Ali imefanyika katika mji alikozaliwa wa Louisville, Kentucky.


Image copyrightGETTY
Image captionBaadhi ya mabondia na muigizaji Will Smith waliohudhuria hafla hiyo.

Umati watu 14000 ulisikiliza kwa makini watu wa tabaka na dini tofauti wakimuomboleza mohammed ali kutokana na umahiri wake katika ulingo wa michezo na pia alivyoitunza jamii, huku wakisifu mchango wake katika kuimarisha amani duniani na haki za binadam.


Image copyrightAP
Image captionUmati wa watu waliohudhuria hafla ya kumbukumbu hiyo

Mkewe Ali, Lonnie Ali, anasema mumewe alikabiliwa na masaibu si haba, bila kuonyesha hasira, na kuwataka watu kufuata mfano wake.


Image copyrightREUTERS
Image captionMkewe Muhammad Ali

Katika taarifa, rais wa Marekani Barrack Obama, alimtaja Ali kama mtu shupavu, aliyeng'aa na aliyekuwa na ushawishi mkubwa kuliko mtu yeyote wa kizazi chake.


Image copyrightREUTERS
Image captionMsafara wa mwili wa Muhammad Ali kabla ya kuzikwa nyumbani Louisvile Kentucky siku ya Ijumaa

Rais wa zamani Bill Clinton, alikumbuka utanashati, ucheshi na utu aliooonyesha marehemu Ali, wakati akikabiliana na machungu ya ugonjwa uliomdhoofisha.

No comments:

Post a Comment