TANGAZO


Sunday, June 19, 2016

Ibada ya Cox imefanyika Birstall


Image copyrightREUTERS
Image captionJo Cox

Ibada ya kumkumbuka mbunge wa Uingereza aliyepigwa risasi na kuuwawa Jo Cox, imefanyika katika makanisa mawili huko Birstall, West Yorkshire.
Askofu Paul Knight amesema kuwa utu wake ulikuwa wenye nguvu isiyo kifani, huku akimtaja kama msamaria mwema wa karne ya 21, aliyekuwa akiwatetea wanyonge na maskini.
Wanaoudhuria maombi hayo ni wanasiasa wengi wa chama cha upinzani cha Labour.
Askofu mkuu wa jimbo la York, Dkt John Sentamu, amesema kuwa Jo Cox, aliuwawa kwa sababu ya kile alichokisimamia, huku akielezea kifo chake kama cha huzuni mkubwa nchini Uingereza.

Image copyrightREUTERS

Kitabu cha maombolezo pia kitafunguliwa kwa wale ambao wanataka kutoa rambirambi zao kwa mwanasiasa huyo, aliyeuwawa siku ya Alhamisi alipokuwa akienda kwenye kituo cha upasuaji, katika eneo bunge lake.
Hapo jana familia ya mbunge huyo, ilifika mahala aliposhambuliwa na kuzingirwa na watu wa Birstall.
Muuwaji wake Thomas Mair, anayetuhumiwa kwa mauwaji hayo alifikishwa mahakamani jijini London hapo jana Jumamosi, na amewekwa kizuizini.

No comments:

Post a Comment