Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Miwgulu Nchemba (kulia) akiongozana na Mbunge wa Busokelo (CCM), Mhe. Atupele Mwakibete kuingia katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuanza vipindi vya asubuhi vya Biunge hilo leo vinavyoendelea mjini Dodoma.
Wabunge wa CCM, Mhe. Hawa Mchafu Viti (Maalum) na Joseph Madaba (Madaba) wakiingia katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuanza vipindi vya asubuhi vya Biunge hilo leo vinavyoendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa Hanang’ Mhe. Mary Nagu akiingia katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuanza vipindi vya asubuhi vya Biunge hilo leo vinavyoendelea mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabulla na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani wakiingia katika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuanza vipindi vya asubuhi vya Biunge hilo leo vinavyoendelea mjini Dodoma.
Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kawekamo Montesori kutoka Jijini Mwanza wakifuatilia mjadala wa vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma.
Mbunge wa Chemba (CCM) (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa asubuhi wa kikao cha Bunge linaloendelea mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe
Na Ismail Ngayonga, Maelezo, Dodoma
10.6.2016
SERIKALI imesema katika mwaka wa fedha 2016/17 itaanza shughuli za utafiti wa maji ya mto rufiji ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa maji katika wilaya za mkoa huo na mkoa wa Dar es Salaam.
Akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Pwani, Hawa Mchafu, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe, alisema mbali na utafiti huo, Serikali pia imekusudia kujenga bwawa la kidunda ili kuhakikisha kuwa wakazi wa miji ya Pwani na Dar es Salaam wanakuwa na maji ya kutosha na yenye uhakika.
Alisema kwa sasa kuna vyanzo viwili vya maji ambavyo ni Ruvu Chini na Ruvu juu, hivyo kukamilika kwa mradi wa maji ya bwawa la kidunda itasaidia kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji.
“Tayari mradi huu upo katika mpango wa Serikali ambapo katika bajeti ya mwaka 2016/17 tayari Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 14 kwa ajili ya bwawa hilo” alisema Kamwelwe
Aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi wa Kidunda utasadia kwa kiasi kikubwa kutosheleza kwa maji katika vyanzo vya maji vya Ruvu juu na Ruvu chini hususani pale ambapo kunapojitokeza vyanzo hivyo kukauka.
Katika Swali lake la nyongeza, Mbunge huyo alitaka kufahamu mkakati wa Serikali wa kutumia maji ya mto rufiji ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji katika wilaya za mkoa wa Pwani.
WAKULIMA WA ZAO LA KOROSHO MKOA WA PWANI WADAI BILIONI 3.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ole Nasha
Na Jonas Kamaleki, Maelezo, Dodoma
10.6.2016
WAKULIMA wa korosho mkoa wa pwani wanavidai vyama vya msingi Tsh. Bilioni 3, madeni ambayo yameorodheshwa na Ofisi ya Mrajis wa vyama vya ushirika nchini.
Hayo yameelezwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ole Nasha wakati akijibu swali la Mbunge wa Ikwiriri (CCM), Mohamed Mchengerwa .
Mbunge wa Ikwiriri alitaka kujua hatua ya Serikali dhidi ya upotevu dhidi ya upotevu wa Tsh. Milioni 900 za wakulima wa korosho.
Mwaka 2012 mrajis wa vyama vya ushirika nchini katika ukaguzi wa vyama vya ushirika vya korosho alibaini upotevu wa Tsh. Bilioni 2 uliosababishwa na Viongozi na Watendaji wa Vyama cya ushirika” alisema.
Kwa mujibu wa Ole Nasha mrajis alibaini kuwa mkoa wa pwani ulikuwa na viongozi 822 wa vyama vya ushirika waliodaiwa kuhusika na upotevu wa fedha hizo.
Aidha Ole Nasha alisema kwa Wilaya ya Rufiji viongozi 41 wa vyama walibainika kufanya ubadhirifu huo na hivyo kwa kutumia kifungu cha 95 cha sheria ya ushirika na. 6 ya mwaka 2013, mrajios aliwaandikia hati ya madai za kuwataka kulipa fedha zlizopotea.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa hadi kufikia mwezi novemba 2015 ni viongozi 790 kati ya 822 wa mkoa wa pwani walikuwa wamerejesha jumla ya Tsh. Milioni 24 na kuongeza kuwa viongozi ambao hawarejesha fedha hizo taratibu zimeandaliwa kuwafikisha katika vyombo vys dola ili hjatua za kisheria ziweze kuchuliwa.
SERIKALI YATUMIA BILIONI 1.5 KULIPA FIDIA KWA WANANCHI WA VIJIJI VYA MWANKONKO NA KISAKI MKOANI SINGIDA.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe.
Na Jonas Kamaleki, Maelezo, Dodoma
10.6.2016
SERIKALI imetumia kiasi cha Tsh. Bilioni 1.5 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wa vijiji vya mwankonko na kisaki mkoani Singida waliopisha miradi ya kuboresha huduma za maji.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe wakati akijibu swali la Mbunge Singida Mjini (CCM) aliyetaka kujua utayari wa Serikali kulipa fidia kwa wananchi wa maeneo ya mwanko na kisaki.
Kamwelwe aliongeza kuwa kiasi cha Tsh. Bilioni 2.9 zinahitajika kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wa maeneo hayo. “Serikali inaendelea na tathimini wa gharama ya fidia hiyo na uhakiki huo ukikamilika fidia zitalipwa” alisema Kamwelwe.
Aidha Kamwelwe alisema kuwa kukamilika kwa mradi wa maji safi mjini Singida kwa sasa kumejitokeza tatizo la kushuka kwa viwango vya uzalishaji maji katika visima viwili vya irao.
Kwa mujibu wa Kamwelwe alisema kutokana na tatizo hilo, Serikali inmechukua hatua za haraka ikiwemo kusafisha visima hivyo na kushusha pampu za visima vyote ili kuongeza kina cha maji.
Akifafanua zaidi alisema baada ya jitihada hizo imeonekana kuwa uwezo wa visima hivyo kutoa maji umeongezeka kwa kiasi na pia Serikali imepanga kubadilisha pampu hizo ili kuongeza uzalishaji wa maji.
HALMASHAURI ZATAKIWA KUKUSANYA CHUPA 450,000 ZA DAMU SALAMA
Na Jonas Kamaleki, Maelezo, Dodoma
10.6.2016
SERIKALI imezitaka Halmashauri za wilaya, manispaa na majiji nchini kukusanya chupa 450,000 za damu ili kukithi mahitaji ya damu salama ya asilimia 1 ya idadi ya watu wote nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini hapa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi ewa habari kuhusu siku ya wachangiaji damu duniani.
“Mwaka huuWizara yagu kupitia mpango wa damu salama inatarajia kuadhimisha siku ya wachangia damu duniani kwa kukusanya angalau chupa 100 za damu kwa kila halmashauri kukusanya chupa 20,000 nchi nzima” alisema Waziri Ummy
Aliongeza kuwa maisha ya watu wengi huokolewa kila siku nchini kwa kuongezewa damu. Kwa mujibu wa Waziri Ummy kina mama wengi na watoto hupoteza maishankwa kukoa damu salama.
Akifafanua zaidi alisema takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa takribani wanawake 432 kati ya wazazi 100,000 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo ya uzazi hapa nchini, ambapo asilimia 80 ya vifo hivyo husababishwa na ukosefu wa damu salama.
Aidha Waziri Ummy alisema ajali za barabarani zitokanazo na bodaboda husababisha vifo na ongezeko kubwa la mahitaji ya damu.
Waziri Ummy alisema takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa ajali za barabarani zimesababisha vifo vya watu 3,468 na kati ya hivyo vifo vya watu 934 vilisababishwa na bodaboda na watu wengine 938 kujeruhiwa.
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia damu kwemnye maadhimisho ya kitaifa yatakayofanyika tarehe 14 Juni mwaka huu mkoani Dodoma na kilele kutanguliwa na kampeni za siku mbili ya kuhamasisha jamii kuhusu uchangiaji damu ka hiari.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Caroline Damian alisema hospitali ya mkoa huo ina uwezo wa kukusanya kiwango cha 75 ya mahitaji ya damu, na kuongeza kuwa jiuhudi za kuwahamasisha wananchi kuchangia damu kwa hiari zinaendelea.
Naye Meneja uendeshaji wa Mpango wa Damu Salama Nchini, Dkt. Abdu Juma alisema mikoa inayoongoza kwa mahitaji makubwa ya damu ni pamoja na Dar es Salaam, Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga, Mara, Kagera na Kigoma.
Alisema sababu za mahitaji hayo ni kutokana na mikoa hiyo kuwa na wingi wa idadi ya watu.



No comments:
Post a Comment