Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) kuongea na wafanyakazi wa BoT leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiongea kwa niaba ya Wakuu wa mikoa ambao mikoa yao ina matawi ya Benki Kuu nchini mara baada ya kuhitimishwa kwa matembezi ya hisani ya wafanyakazi BoT yaliyoanzaia kutoka makao makuu ya Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam, matembezi hayo yalikuwa na lengo la kuchangia ununuzi wa madawati ya shule za msingi na sekondari kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) mfano wa hundi ya Sh. 273,089,338 leo jijini Dar es salaam kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuchangia ununuzi wa madawati.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akionesha mfano wa hundi ya Sh. 273,089,338 aliyokabidhiwa na Benki Kuu leo jijini Dar es salaam ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuchangia ununuzi wa madawati.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kulia) akimpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) mara baada ya kuongea na wafanyakazi wa Benki Kuu (BoT) (hawapo pichani) baada ya kuhitimisha matembezi ya hisani ya wafanyakazi hao leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki Kuu (BoT) wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) mara baada ya kuhitimisha matembezi ya hisani ya wafanyakazi hao kutoka makao makuu ya Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam yaliyokuwa na lengo la kuchangia ununuzi wa madawati ya shule za msingi na sekondari kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki.

Mmoja wa Wafanyakzi wa Benki Kuu ya Tanzania Gloria Mahina akicheza kufurahia wimbo ulioimbwa na kwaya ya muungano wa wafanyakazi wa BoT kutoka matawi yote nchini ikijumuisha mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Zanzibar, Dodoma na Mtwara.
Kwaya ya muungano wa wafanyakazi wa BoT kutoka matawi yote nchini ikijumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Zanzibar, Dodoma na Mtwara ikitumbiza baada ya kuhitimisha matembezi ya hisani ya wafanyakazi hao kutoka makao makuu ya Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika moja ya banda kujionea shughuli zinazofanywa na Benki kuu ya Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Benki kuu ya Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Benki kuu ya Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Na Hussein
Makame-MAELEZO
BENKI Kuu ya Tanzania
(BOT) na wafanyakazi wake wa matawi yote nchini kwa kushirikana na baadhi ya Taasisi
za kifedha na kampuni za simu nchini, imetoa Shilingi Milioni 273 kuchangia
ununuzi wa madawati ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Benki hiyo.
Fedha hizo zilikabidhiwa
leo kupitia hundi ya mfano kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya matembezi
ya hisani yaliyolenga kuchangia madawati, yaliyoanzia Ofisi za BOT hadi kwenye
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza kabla ya
kukabidhi fedha hizo, Gavana wa BOT Prof. Benno Ndulu alisema lengo la mchango
huo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuongeza ubora
wa elimu kupitia upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari nchini.
“Tunatambua kwamba
changamoto hiyo (uhaba wa madawati) ni kubwa, lakini tunaamini mchango wetu
utasaidia kupunguza makali ya tatizo hilo na kuongeza idadi ya watoto wetu
ambao wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati” alisema Gavana Prof. Ndulu.
Akifafanua mchango
huo, Gavana Prof. Ndulu alisema kati ya fedha hizo, BOT imetoa Shilingi Milioni
167, Wafanyakazi Milioni 29.8, Taasisi za Kifedha Milioni 22 na kampuni za simu
Milioni 54.3 na kwamba madawati hayo yatasambazwa kwenye shule zenye upungufu
au ukosefu wa madawati za Dar es Salaam na zilizoko mikoa ambayo Benki hiyo ina
matawi yake.
Alitaja mikoa hiyo na
fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa BOT wa matawi ya mikoa hiyo kuwa ni Makao
Makuu Dar es Salaam waliochangia Shilingi Milioni 22, Mwanza (Milioni 1.24),
Chuo cha Benki Mwanza (680,000) Arusha (Milioni 1.23) Mbeya (Milioni 1.186),
Mtwara (850,000) na Dodoma (Milioni 1.18).
Alisema taasisi
zilizochangia fedha hizo ni Benki ya India Shilingi Milioni 5, Benki ya Habib
(Milioni 5), Benki ya Exim (Milioni 5), Benki ya UBA (United Bank for Africa, Milioni
2), Tanzania Mortgage Refinance (Milioni 2), China Community Bank (Milioni 2)
na NIC Bank aliyotoa Milioni 1.
Kwa upande wa kampuni
za simu zilizotoa fedha ni kampuni ya Vodacom iliyotoa Dola za Kimarekani
10,000, kampuni ya Tigo Dola za Kimarekani 10,000 na kampuni ya Selcom iliyotoa
Dola za Kimarekani 5,000.
Akizungumza baada ya
kupokea hundi ya mfano, Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza fedha hizo zitumike
kama zilivyokusudiwa na yeyote atakayetumia fedha hizo kinyume na malengo
achukuliwe hatua mara moja.
Katika kuthamini
sekta ya elimu nchini, Gavana Prof. Ndulu alisema benki hiyo ilianzisha Mfuko
wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo hadi sasa umetoa ufadhili
kwa wanafunzi 22 kusoma shahada za kwanza na za uzamivu katika vyuo vikuu hapa
nchini katika masomo ya sayansi, hisabati, uchumi, fedha, uhasibu na TEHAMA.
“Lengo kubwa la mfuko
huu ni kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi na hisabati
yakiwemo masomo kuhusu gesi na mafuta.Katika idadi hiyo, 16 ni wanafunzi wa
kike na waliobaki 8 ni wanaume” alisema Gavana Prof. Ndulu.
Benki Kuu ya Tanzania
(BOT) ilianza kutoa huduma kwa wananchi mnamo tarehe 14 Juni mwaka 1966 na Juni
14 mwaka huu inatimiza Miaka 50 na katika kuadhimisha miaka hiyo wafanyakaz wa
matawi yote nchini wanafanya matembezi hayo ili kutoa mchango kwa jamii.

No comments:
Post a Comment