Pages

Thursday, May 5, 2016

WATUMISHI WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO WAPATA MAFUNZO YA MATUMIZI MAZURI YA HUDUMA ZA MAWASILIANO YA KIJAMII

Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandishi James Kilaba (kushoto) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Khalfani Mrisho wakati walipotembelea ofisi hizo kwa ajili ya mafunzo mafupi ya matumizi ya huduma za mawasiliano na mitandao ya kijamii yanayotolewa kwa watumishi wa wizara hiyo. Wengine Pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, wizara hiyo, Bw. Mkapana Bi Zawadi Msalla ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wizarani hapo.
Meneja Mawasiliano Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Innocent Mungy akitoa mada ya ukuaji wa sekta ya mawasiliano na changamoto zake kwa watumishi wa umma kutoka wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mamlakaya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandishi James Kilaba akizungumza na watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (hawapo pichani), wakati wa mafunzo mafupi ya matumizi ya huduma za mawasiliano na mitandao ya kijamii jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakifuatilia kwa karibu mafunzo ya Matumizi Mazuri ya huduma za Mawasiliano na mitandao ya kijamii iliyotolewa leo hii na Mamlaka ya Utangazaji Tanzania.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Khalfani Mrisho akitoa hotuba ya kufungua mafunzo mafupi ya matumizi ya huduma za mawasiliano na mitandao ya kijamii yanayotolewa kwa watumishi wa wizara ya hiyo na Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

No comments:

Post a Comment