Mkufunzi wa kilabu ya Manchester City Louis van Gaal ana matumaini ya kusalia katika kilabu hiyo msimu ujao.
Raia huyo wa Uholanzi hajapewa thibitisho lolote kuhusu hatma yake lakini ana matumaini ya kuendelea kuhudumu kwa mwaka wa mwisho wa kandarasi yake ya miaka mitatu aliyotia saini mwaka 2014.
Alisema:Nimesema nitakuwa hapa,hayo ni maoni yangu kwa hivyo ni bodi kuamua iwapo nitasalia au la.
Van Gaal amekuwa na shinikizo kali tangu mwezi Disemba na aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho anaaminika kufanya mazungumzo na maafisa wa Manchester United.
United ambao walitangaza matokeo ya kifedha ya robo mwaka na ambao wanatarajia kupitisha mapato ya pauni 500 mwaka huu,wanajua kwamba hawatashiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha misimu mitatu iwapo Manchester City itazuia kushindwa katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Swansea siku ya Jumapili.
No comments:
Post a Comment