Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake kuhusu kasi ya kuimarika kwa ushirikiano kati ya kundi la wapiganaji la Boko Haram nchini Nigeria na lile la Islamic State, wakati Nigeria inaandaa kongamano la kupambana na kundi hilo la kigaidi.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, baraza hilo la wanachama 15 limesema kuwa Boko Haram linaendelea kuwa tishio kwa amani na usalama wa mataifa ya Afrika Magharibi na Afrika ya kati.
Boko Haram lilitangaza utiifu wake kwa Islamic State mwaka jana, na inaripoitiwa kuwa liliwatuma wapiganaji wake kuungana na Islamic State nchini Libya.
Baraza hilo pia limekaribisha kongamano lililoandaliwa na rais wa Nigeria Mohamadu Buhari siku ya Jumamosi, kuangazia upya jitihada za kupambana na wapiganaji hao.
Kongamano hilo litahudhuriwa na viongozi wa kikanda pamoja na rais wa ufaransa Francois Hollande.
No comments:
Post a Comment