Kumetokea shambulizi la kujitolea Mhanga katika kiwanda cha gesi kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
Ripoti zinasema kuwa takriban watu 11 wameuwawa na wengine 20 wamejeruhiwa vibaya.
Msemaji wa jeshi la Iraq anasema gari lililokuwa limetegwa vilipuzi lililipuka karibu na lango la kiwanda hicho.
Baadaye washambuliaji sita wa kujitolea kufa wakaingia ndani ya kiwanda hicho ambapo walikabiliana na maafisa wa uslama.
Matenki ya gesi pia yamewashwa moto.
No comments:
Post a Comment