Pages

Tuesday, May 31, 2016

SERIKALI KUANZISHA BENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazotoka viwandani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazotoka viwandani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiongea na wadau wa sekta ya Viwanda wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 na kuwataka kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo ya shirikisho la viwanda nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga na wa pili ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wadau wa sekta ya viwanda nchini(hawapo pichani) na kuwaahidi kuwaunga mkono katika harakati za kuendeleza sekta ya viwanda ikiwamo kuanzisha banki ya maendeleo ya viwanda nchini itakayosaidia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wale wenye nia ya kuanzisha viwanda. 
Wadau wa Sekta ya Viwanda nchini wakimsilkiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.

Na Lilian Lundo-MAELEZO
SERIKALI ya awamu ta Tano imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya sasa.

Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema kuwa jambo hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi yetu ina rasilimali zinazohitajika katika kujenga uchumi wa viwanda.

“Nafahamu kwamba tunakila aina ya rasilimali inayowezesha uwepo wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa kutosha pamoja na malighafi zake na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuifanya sekta ya viwanda kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli aliwatoa wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la uhakika kwa bidhaa zitakazozalishwa kwani Tanzania imezungukwa na nchi zenye uhitaji wa bidhaa mbalimbali na pia ni Mwanachama wa jumuiya mbalimbali ndani na nje ya Afrika.

Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage aliwataka wamiliki wa Viwanda Nchini kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.

No comments:

Post a Comment