Afisa wa ukaguzi katika shirikisho la soka duniani Fifa Domenico Scala,amejiuzulu akipinga mabadiliko yanayofanyika katika shirikisho hilo.
Scala amekasirishwa na hatua ya Baraza jipya la Fifa lenye uwezo wa kuajiri na kuwafuta kazi wale wanaosimamia kamati zake ikiwemo ile ya ukaguzi,maadili na fedha.
Baraza hilo lilichukua mahala pa kamati kuu ya Fifa kufuatia madai ya ufisadi katika shirikisho hilo.
''Kamati hizo sasa zitakuwa hazina uhuru kutekeleza majukumu yake'',alisema Scala.
Ameongezea kuwa: Hatua hiyo inahujumu nguzo ya uongozi mzuri wa Fifa na inaharibu ufanisi wa mabadiliko yaliofanywa.
Scala alikuwa na jukumu muhimu katika kusukuma mabadiliko kufuatia kashfa iliolazimu kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter na mwenzake wa Uefa Michel Platini.
No comments:
Post a Comment