TANGAZO


Sunday, May 8, 2016

CRDB BANK YAHIMIZA WATANZANIA KUWEKEZA KWENYE HISA

 
Wakurugenzi wa Matawi ya Benki ya CRDB wakifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa PPR, wakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana . Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Kijitonyama, Lucas Msigazi, Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Kibaha, Rosemary Nchimbi, Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba, Pendo Assey, na Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Vijana, Peres Fungo. Semina hiyo ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika mjini Arusha, Tarehe 21 ya mwezi huu. 
Wakurugenzi wa Matawi ya Benki ya CRDB wakibadilishana mawazo, wakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba, Pendo Assey, Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Kijitonyama, Lucas Msigazi, naMkurugenzi wa CRDB Tawi la Kibaha, Rosemary Nchimbi. Semina hiyo ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika mjini Arusha, Tarehe 21 ya mwezi huu.

Wakurugenzi wa Matawi ya Benki ya CRDB  wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Kijitonyama, Lucas Msigazi, Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Kibaha, Rosemary Nchimbi,Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba, Pendo Assey, na Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Vijana,Peres Fungo. Semina hiyo ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika mjini Arusha, Tarehe 21 ya mwezi huu.
Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba, Pendo Assey, na Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Vijana, Peres Fungo wakimsikiliza Ofisa wa Benki ya CRDB, Tawi la Lumumba, Vivian Marwa wakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika mjini Arusha, Tarehe 21 ya mwezi huu.
Maofisa wa Benki ya CRDB Tawi la Lumumba,  Vivian Marwa na Calist Temba, wakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika mjini Arusha, Tarehe 21 ya mwezi huu.
Mkurugenzi wa  CRDB Tawi la Vijana, Peres Fungo akizungumzawakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana . Semina hiyo ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika mjini Arusha, Tarehe 21 ya mwezi huu.
Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba, Pendo Assey, na Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Vijana, Peres Fungo wakibadilishana mawazo, wakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika mjini Arusha, Tarehe 21 ya mwezi huu.
Mkurugenzi wa  CRDB Tawi la Lumumba, Pendo Assey akizungumza wakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika mjini Arusha, Tarehe 21 ya mwezi huu.

Baadhi ya Maofisa wa Benki ya CRDB Tawi la Lumumba, wakifuatilia  semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika mjini Arusha, Tarehe 21 ya mwezi huu. 

Na Mwandishi wetu
BENKI ya CRDB, imewahimiza Watanzania  wanao  tumia mabenki kuweka fedha zao za akiba, wasiishie kwenye kuweka akiba tuu, bali watumie sehemu ya akiba zao kwa kuziwekeza kwenye ununuzi wa hisa hivyo kupata fedha kubwa zaidi, kuliko kujiwekea akiba pekee. 

Wito huo, umetolewa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Tawi la Vijana, Peres Fungo, na Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba, Pendo Assey, , wakati wa semina ya uhamasishaji uwekezaji, kwa wanahisa wa benki ya CRDB, kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika baadae mwezi huu, mjini Arusha.

Akifafanua kuhusu kuweka akiba na kununua hisa, Mkurugenzi Fungo amesema fedha ukiziweka akiba benki, unazitunza fedha zako zinakuwa salama na huku zinazalisha faida.  , lakini ukitumia sehemu ya akiba, kwa kuiwekeza kwenye ununuzi wa hisa, unakuwa umejiwekea akiba lakini wakati huo huo pia unazalisha faida kubwa zaidi kwa kulipwa gawio ambalo siku zote kiwango chake ni kikubwa kuliko kiwango cha riba ya akiba pekee.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Lumumba, Pendo Assey mabenki yote yanatoa huduma zinazofanana tofauti kati ya benki moja na nyingine ni jinsi benki husika inavyomhudumia mteja, lakini kwa upande wa CRDB Banki, Bibi Assey amesema  “CRDB ni benki inayomsikiliza sana mteja, sio tuu kwa kumhudumia mteja kile benki inachotoa, bali kwa kumsikiliza mteja na kumpa huduma mteja anayotaka ambako kumepelekea CRDB  kufurikwa na wateja.

Mkurugenzi wa CRDB Tawi la Kijitonyama, Lucas Msigazi aliwahimiza wanahisa wa CRDB Bank kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo, ili kuyasikia maendeleo ya benki yao, na kuishauri wanataka benki iwafanyie nini kuboresha huduma zake.

Naye Meneja wa CRDB Tawi la Kibaha, Rosemary Nchimbi, alisisitizia umuhimu wa mkutano huo, na kueleza wale watakaoshindwa kuhudhuria, watawatumia wanahisa wengine kuwawakilisha na kuwakilisha mawazo yao.

Mkutano huo wa wanahisa wa Benki ya CRDB utakaofanyika Tarehe 21 mwezi May, utakwenda sambamba na kio ya maadhimisho ya mafanikio ya CRDB katika kipindi cha miaka 20 ya uwepo wake, ambapo benki hiyo imefanikiwa kuwafikishia huduma za kifedha Watanzania walio wengi na haswa walio vijijini, hivyo CRDB kujikuta imetimiza malengo ya kuanzishwa kwake.  

No comments:

Post a Comment